FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, jana Aprili 26 aliambulia kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Biashara United ya Mara. Kocha huyo ...
FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, jana Aprili 26 aliambulia kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Biashara United ya Mara.
Kocha huyo ambaye amejiunga na Kagera Sugar akitokea Biashara United mbinu zake kwa timu yake ya zamani zilikwama na kushuhudia akiyeyusha pointi tatu mazima, Uwanja wa Karume, Mara.
Unakuwa ni mchezo wa nne kwa Baraza kushindwa kufurukuta kupata pointi tatu baada ya kubeba mikoba ya Mecky Maxime ambaye alifutwa kazi ndani ya Kagera Sugar kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo.
Ni Deogratius Mafie dakika ya 24 na Lenny Kissu dakika ya 28 walitupia kwa upade wa Biashara United huku lile la kufuta machozi kwa Kagera Sugar likipachikwa kimiani na Vitalis Mayanga dakika ya 84.
Matokeo hayo yanaifanya Kagera Sugar kubaki na pointi zake 27 ipo nafasi ya 16 ikiwa imecheza jumla ya mechi 28, Biashara United imezidi kujijengea ngome nafasi ya nne baada ya kufikisha jumla ya pointi 44.
Kagera Sugar haijawa na mwendo mzuri msimu huu ambapo ipo kwenye mstari mwekundu ambao ni wa kushuka daraja kwenda Ligi Daraja la Kwanza.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS