MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo wanatarajiwa kukwea pipa kuanza kuwafuata wapinzani wao Al Ahly kwa ajili ya mchezo wa Li...
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo wanatarajiwa kukwea pipa kuanza kuwafuata wapinzani wao Al Ahly kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kupitia Dubai.
Safari ya wawakilishi hao wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika inatarajiwa kuanza leo Aprili 6 majira ya saa 9:25 alasiri ambapo kitaibukia Dubai.
Leo kitaondoka Dar mpaka Dubai, kitapumzika hapo na Aprili 7 kitaondoka Dubai kwenda kwa Waarabu wa Misri.
Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa wanakwenda kuwakabili Al Ahly wakiwa na imani kwamba watapata pointi tatu muhimu.
"Kila kitu kipo sawa na kwa sasa Simba ni timu kubwa kwa kuwa ipo ndani ya timu 8 bora kwa hiyo tunakwenda kudhihirisha hilo kwa vitendo.
"Ushindani ni mkubwa na kila mmoja anahitaji kuona timu inapata ushindi hilo nalo linatupa nguvu ya kwenda ugenini tukijiamini,".
Timu zote mbili zimetinga hatua ya robo fainali, Simba ina pointi 13 na Al Ahly ina pointi 8 katika kundi A.
Zilipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Simba 1-0 Al Ahly ambapo bao la Simba lilipachikwa na Luis Miquissone kwa pasi ya Clatous Chama.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS