Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) Yafanya Ziara Mbeya
HomeHabari

Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) Yafanya Ziara Mbeya

BODI ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mej.Gen(Mstaafu) Hamisi Semfuko i...

Serikali Ya Tanzania Yaanika Sababu Ya Kuwa Na Simba Wengi Duniani
Rais wa Burkina Faso Roch Marc Christian Kaboré azuiliwa katika kambi ya kijeshi
Mkawe Na Ushawishi Kwa Wananchi Ili Wajitokeze Kupata Huduma Ya Chanjo- Prof. Makubi


BODI ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mej.Gen(Mstaafu) Hamisi Semfuko imetembelea Pori la Akiba la Mapanga /Kipengere lililopo katika Mkoa wa Njombe na Mbeya na kufanya kikao na watumishi wa pori hilo.

Katika Safari hiyo Mwenyekiti wa Bodi aliambatana na Menejimenti ya TAWA ikiongozwa na Kamishna wa Uhifadhi Bw. Mabula Nyanda Misungwi pamoja na Naibu Kamishna wa Huduma za Utalii na Biashara Bw. Imani Nkuwi na uongozi wa Pori hilo uliongozwa na Meneja wa Pori Bw.Joas Makwati.

Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA Mej.Gen (Mstaafu) Hamisi Semfuko akiongea  wa watumishi wa Poria Akiba  Mpanga/Kipengere aliwaelezea kuwa Lengo la safari yake na wajumbe wa Bodi ni kufanya ukaguzi wa uendelezaji miradi ya maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya utalii na ufuatiliaji wa utelelezaji kazi.

Ameongeza kuwa Lengo ikiwa ni kuimarisha uhifadhi wa rasilimali za wanyamapori, kuongeza watalii na mapato na kuboresha utendaji wa Shirika.

Meneja wa Pori hilo Joas Makwati,alimueleza Mwenyekiti na msafara wake kuwa kuna, vivutio vya utalii, kwa Kuwepo kwa aina mbalimbali za Wanyamapori pia kuna maporomoko 7 ya maji ikiwemo Kimani ambayo ni maarufu, ya kuvutia na ya kipekee katika ukandaa wa kusini mwa Tanzania.

Aidha pia  Ukanda wa maua na nyasi na miinuko na mabonde yanaifanya Hifadhi  hiyo kuwa na mandhari nzuri.

Hata hivyo  meneja huyo alimweleza Mwenyekiti wa Bodi kuwa Hifadhi hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazosabisha kutofikiwa malengo mahususi ya kuanzishwa Kwake ikiwemo,upungufu wa watumishi na  Ukosefu wa kambi za kitalii na barabara za kuvifikia vivutio.

kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi aliwakumbusha watumishi kufanya kazi kwa nidhamu, weledi, uadilifu na kutojihusisha na vitendo vya rushwa.

Pia  amesema kuwa amefurahishwa na mawazo chanya yaliyowasilishwa Kwame yenye lengo la kuijenga Taasisi na kuifanya ipige hatua na hivyo kuwahakikishia kuwa maoni yao yamepokelewa na yatafanyiwa kazi kwa haraka ili kuleta tija kwa Shirika akishirikiana na Menajimenti ya TAWA.

Baada ya kikao hicho Mwenyekiti na msafara wake wakitembelea Maporomoko ya maji ya Kimani ambayo ni  maarufu  kutokana na maji yake kuanguka katika umbo la ngazi ngazi kwa  umbali wa mita zaidi ya 70 na yanapoanguka ya natengeneza  mvuke

Pia baada ya kuona Maporomoko ya maji ya Kimani alihitimisha safari yake Kwa kutembelea pango la Mtemi Mkwawa.

Pango hili linasadikiwa kutumiwa na Mtemi Mkwawa Kwa ajili ya mapumziko/Maficho kipindi cha vita ya wahehe na wajerumani.Pango lipo jirani na Maporomoko ya maji ya mto Kimani


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) Yafanya Ziara Mbeya
Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) Yafanya Ziara Mbeya
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj-kLHMiA6xOK77RQO2QWWOqVhyphenhyphenWgR3Rq0PN5rFG3hspUzi8GYvGx1A__m6kxLSDCeAA9hXhRH0tsHz_1vhqBSXq6AWDg5e-a6jz00jrQaTKHn_fMs3j6y2yLVKKw-zQj3JUJtRfg57UaLu/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj-kLHMiA6xOK77RQO2QWWOqVhyphenhyphenWgR3Rq0PN5rFG3hspUzi8GYvGx1A__m6kxLSDCeAA9hXhRH0tsHz_1vhqBSXq6AWDg5e-a6jz00jrQaTKHn_fMs3j6y2yLVKKw-zQj3JUJtRfg57UaLu/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/bodi-ya-wakurugenzi-wa-mamlaka-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/bodi-ya-wakurugenzi-wa-mamlaka-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy