Mkawe Na Ushawishi Kwa Wananchi Ili Wajitokeze Kupata Huduma Ya Chanjo- Prof. Makubi
HomeHabari

Mkawe Na Ushawishi Kwa Wananchi Ili Wajitokeze Kupata Huduma Ya Chanjo- Prof. Makubi

Na. WAF- Morogoro Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Waratibu wa Chanjo ngazi za Mikoa na ...

Watu 9 wamefariki katika ajali ya boti Zanzibar
Mataifa makubwa kinyuklia yaahidi kupunguza silaha za nyuklia
Rais wa Msumbiji na mke wake wamekutwa na corona


Na. WAF- Morogoro
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Waratibu wa Chanjo ngazi za Mikoa na Wilaya kuwa na ushawishi kwa wananchi ili kujitokeza kwa wingi kupata huduma ya chanjo dhidi ya UVIKO-19.

Prof. Makubi ameyasema hayo  tarehe 23/1/2022 alipokuwa akifunga mkutano wa tathmini ya huduma za chanjo ngazi ya Mikoa/Wilaya uliofanyika kwa siku Tatu katika manispaa ya Morogoro.

“Niwaombe sana Waganga Wakuu wa Mikoa mkawe na ushawishi mzuri, chanjo zisiwe zinabaki Mikoani au wilayani mkazitoe kwa kuwapatia wananchi huduma.”amesema Prof. Makubi

Aidha, Prof. Makubi amesisitiza kuwa na uwajibikaji mzuri kazini kwa kuwa baadhi ya watendaji hawafanyi vizuri katika uongozi wao.

“Kuna baadhi ya viongozi hamfanyi vizuri, mkajirekebishe Kuna malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali juu ya utendaji wenu.”Almesisitiza Prof. Makubi

Amesema Serikali inajitahidi kutoa sapoti kwa kutoa vifaa na fedha ili watendaji wakafanikiwe katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.

Pia amesema ombi la Waratibu hao wa chanjo wa Mkoa/Wilaya kuwapatia usafiri wa pikipiki litafanyiwa kazi ili kurahisisha majukumu yao ya huduma tembezi za chanjo na zile za kila siku katika maeneo yao ya kazi. Kwa sasa tayari Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan umenunua magari zaidi ya 200 kwa ajili ya waganga Wakuu Wilaya Wote nchini.

Hata hivyo Prof. Makubi ameipongeza Mikoa inayofanya vizuri katika uchanjaji wa UVIKO-19 ikiwemo Ruvuma, Mara na Mwanza. “Naagiza mikoa mingine kujifunza mbinu na mikakati iliyotumika kwenye mikoa hii ili waweze kuitumia kuleta mafanikio katika mikoa yao.”amesema Prof. Makubi

Malengo ya mkutano huo yalikuwa ni kupitia taarifa za utekelezaji wa huduma za chanjo kwa mwaka 2021, kutambua mafanikio na changamoto na kuweka mipango ya kuboresha zaidi huduma za chanjo kwa mwaka 2022.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mkawe Na Ushawishi Kwa Wananchi Ili Wajitokeze Kupata Huduma Ya Chanjo- Prof. Makubi
Mkawe Na Ushawishi Kwa Wananchi Ili Wajitokeze Kupata Huduma Ya Chanjo- Prof. Makubi
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEghRtt0ez9hVSByJ78WizF7-z29C-e8aukhgj64sKy5pFXHB2Eqf7m6Fjce7093FDILjhiuhsdQfyPw_Duoc0oEprcOsLHb7FKRp_PAWs2EiAMZFtHcq4h-eT08bnyBAfquHYdr0ocqRFzSdtJgWVYheTBqPRbndr3zp6jRvBUcHV-T24loGl7Du5Cr0g=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEghRtt0ez9hVSByJ78WizF7-z29C-e8aukhgj64sKy5pFXHB2Eqf7m6Fjce7093FDILjhiuhsdQfyPw_Duoc0oEprcOsLHb7FKRp_PAWs2EiAMZFtHcq4h-eT08bnyBAfquHYdr0ocqRFzSdtJgWVYheTBqPRbndr3zp6jRvBUcHV-T24loGl7Du5Cr0g=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/mkawe-na-ushawishi-kwa-wananchi-ili.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/mkawe-na-ushawishi-kwa-wananchi-ili.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy