Serikali Ya Tanzania Yaanika Sababu Ya Kuwa Na Simba Wengi Duniani
HomeHabari

Serikali Ya Tanzania Yaanika Sababu Ya Kuwa Na Simba Wengi Duniani

Na Mwandishi Maalum, Las Vegas,Marekani. RAIS wa Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa, (SCI), Sven Lindqueast ameitaja Tanzania kuwa ni nchi...


Na Mwandishi Maalum, Las Vegas,Marekani.

RAIS wa Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa, (SCI), Sven Lindqueast ameitaja Tanzania kuwa ni nchi yenye  nusu ya simba wote Duniani katika Mkutano wa 50 wa Mwaka wa Uwindaji wa Kitalii unaoendelea kufanyika nchini hapa.


Rais huyo Bw. Sven Lindquest amesema kwa hatua hiyo ameipongeza kwa juhudi za utunzaji na kupelekea wingi wa wanyama hao.

Kwa upande wake Serikali kupitia Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ametaja sababu zilizopelekea nchi ya Tanzania kutajwa kuwa nchi yenye Simba wengi Duniani licha ya kuruhusu uwindaji wa kitalii.


Akizungumza leo  katika  Jijini la  Las Vegas nchini Marekani, Dkt.Ndumbaro amesema nusu ya simba wote wapo Tanzania  kutokana na uimara wa serikali ya Tanzania katika shughuli za  uhifadhi

Amesema kuimarika kwa shughuli za uhifadhi hususani kwa Wanyamapori walao nyasi ni moja ya sababu ya Tanzania kuwa na Simba wengi  hivyo imepelekea  Simba nao  kuongezeka kutokana na uhakika wa  chakula cha kutosha


Amefafanua kuwa Simba hula wanyamapori walao nyasi na wanyamapori hao walao nyasi wamekuwa wengi kutokana na uwepo wa nyasi za kutosha kutokana na usimamizi bora wa maeneo ya Hifadhi


" Kubadilishwa  mfumo kutoka wa kirai kwenda katika mfumo wa kijeshi kwa Watumishi wote wanaosimamia maeneo ya Hifadhi ni moja ya sababu ya simba kuongezeka kwa Simba nchini Tanzania" alisema Dkt.Ndumbaro


Waziri  Ndumbaro  amesisitiza kuwa Tanzania imefanikiwa kuwa simba wengi kutokana na serikali kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha shughuli za uhifadhi nchini kwa kuitengea Wizara ya Maliasili na Utalii bajeti ya kutosha inayotumika katika kuendesha operesheni mbalimbali za kukabiliana na ujangili


Amesema hadi sasa Serikali imeweza kufanikiwa kukomesha tatizo hilo la  ujangili kwa  zaidi ya asilimia 90 na kusisitiza kuwa ifikapo 2025 itarajia kumaliza kabisa tatizo la  ujangili kwa kufikia asilimia 100%


" Uthubutu wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan wa kuwa bega kwa bega na Wizara imekuwa chachu kwa Tanzania kuzidi kuongoza kwa kuwa na simba wengi Duniani" amesisitiza Dkt Ndumbaro


Pia, Dkt.Ndumbaro ameitaja sababu nyingine kuwa ni utolewaji wa elimu kwa Jamii,  amesema kwa sasa Jamii imetambua umuhimu wa wanyamapori hivyo wananchi wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa serikali  kwa kutoa taarifa vitendo vya ujangili vinapotokea.


" Kama nchi tumejiwekea utaratibu wa kuhakikisha wananchi wote wanaoishi katika maeneo ya Hifadhi wananufaika kwa kusogezewa huduma za kijamii, hivyo Jamii imekuwa inaona faida ya moja kwa moja ya uwepo wa  wanyamapori" alisisitiza Dkt. Ndumbaro


Katika hatua nyingine, Dkt. Ndumbaro amesema  uwepo wa sheria kali ya  kutokuruhusu shughuli za kibinadamu kuendeshwa ndani ya maeneo ya Hifadhi kumepelekea maeneo ya Hifadhi kubaki katika uasili wake hivyo  simba wamezidi kuongezeka kutokana uwepo mazingira salama ya wanyamapori wengine


Aidha, Dkt.Damas Ndumbaro amesema licha ya Tanzania kuwa na vitalu vya uwindaji wa kitalii zaidi ya 100 lakini imekuwa  ikiendesha Uwindaji huo  kwa kuzingatia  matumizi  endelevu ndio maana imezidi kuongoza Duniani kwa kuwa na simba wengi

Kufuatia hali hiyo, Dkt. Ndumbaro amekanusha madai ya baadhi ya nchi zinazopinga  Uwindaji wa Kitalii kwa kisingizio kuwa utalii huo umekuwa ukipunguza idadi ya wanyamapori ambapo amesisitiza kuwa Uwindaji wa Kitalii ni muhimu kwa kuwa umekuwa ukisaidia kupunguza idadi ya wanyamapori waliozidi ili kupunguza athari kwa binadamu


Amesema kwa sasa nchini Tanzania kumekuw athari kwa binadamu kutokana na ongezeko la  Wanyamapori kama vile tembo pamoja na mamba

 Mwisho.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Serikali Ya Tanzania Yaanika Sababu Ya Kuwa Na Simba Wengi Duniani
Serikali Ya Tanzania Yaanika Sababu Ya Kuwa Na Simba Wengi Duniani
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjnqhblDI_11HS0rpnTZv9x17Yg3H8PMRh9LmMZ6yNCHK2JZSj_TlLp9w1c7jHTpLh-8bhk68DJtmZ6XElhH_iqqt-lPx5yIyYVp3zlNABwalvjAemrspQa0Y6Ecsfb9WOpPcuUcx-eA2jqheQQf-1G9FAAmNc8ThFCho0vwpCJsJmIs9_Jinfyt9AfGg=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjnqhblDI_11HS0rpnTZv9x17Yg3H8PMRh9LmMZ6yNCHK2JZSj_TlLp9w1c7jHTpLh-8bhk68DJtmZ6XElhH_iqqt-lPx5yIyYVp3zlNABwalvjAemrspQa0Y6Ecsfb9WOpPcuUcx-eA2jqheQQf-1G9FAAmNc8ThFCho0vwpCJsJmIs9_Jinfyt9AfGg=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/serikali-ya-tanzania-yaanika-sababu-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/serikali-ya-tanzania-yaanika-sababu-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy