BEKI MPYA YANGA:NITAFANYA MAKUBWA
HomeMichezo

BEKI MPYA YANGA:NITAFANYA MAKUBWA

INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Yanga, beki wa kati kijana Dickson Job amesema kuwa anaamini atafanya makubwa ndani ya kikosi hicho kinac...

JEMBE: KIPA POLISI TANZANIA LAZIMA AHOJIWE
UEFA YAPIGA KUANZISHWA KWA EUROPEAN SUPER LEAGUE
SABABU YA DILI YA SABILO KUBUMA YANGA NI KOCHA MBELIGIJI

INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Yanga, beki wa kati kijana Dickson Job amesema kuwa anaamini atafanya makubwa ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze. 

Job ameibukia ndani ya Yanga akitokea Klabu ya Mtibwa Sugar na amesaini dili la miaka miwili kuwatumikia Wanajangwani ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara. 

Yanga inaongoza ligi baada ya kucheza jumla ya mechi 18 na kibindoni imekusanya jumla ya pointi 44 na haijapoteza mchezo mpaka sasa.

Maisha yake ndani ya Mtibwa Sugar msimu wa 2020/21 yalikuwa yenye furaha na alikuwa na uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza. Katika mechi 18 ndani ya Mtibwa Sugar alicheza 17 na zote aliyeyusha dakika 90 huku akikosekana kwenye mchezo mmoja mbele ya Mbeya City. 

Tayari ameanza maisha mapya ndani ya Yanga huku akiwa na furaha pia kwa kuwa anatimiza ndoto yake ya muda mrefu kwani alikuwa anafikiria kucheza ndani ya timu hiyo jambo ambalo limetimia.

Job amesema:-"Ninafurahi kuwa Yanga nina amini kuwa nitafanya mambo makubwa, ilikuwa ni ndoto yangu kucheza ndani ya Yanga na sasa imetimia.

"Kikubwa ni kufuata maelekezo ya benchi la ufundi, ushirikiano na wachezaji wenzangu pamoja na kufanya kazi bila kusahau ibada hapo nina amini kwamba kila kitu kitakwenda sawa," .

Anafanya jumla ya mabeki wa kati ndani ya Yanga kwa sasa kuwa watano ambapo ni pamoja na Lamine Moro huyu ni raia wa Ghana, Bakari Mwamnyeto, Said Juma, Abdalah Shaibu pamoja na yeye mwenyewe Job.



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: BEKI MPYA YANGA:NITAFANYA MAKUBWA
BEKI MPYA YANGA:NITAFANYA MAKUBWA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiL12SNcMkxeOqvnbhU79bsZw6yIJ5GnPPCrPOwNxqlCiSipFA4shQXLO8nrxMpUmx8qyTObcrUG3T2e_83hp_Q90cIPam-hwRafdRMDtvajDxDlDp-3ItJ7ml_lInKst2zaFDQEZvvyZAQ/w512-h640/IMG_20210129_083558_436.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiL12SNcMkxeOqvnbhU79bsZw6yIJ5GnPPCrPOwNxqlCiSipFA4shQXLO8nrxMpUmx8qyTObcrUG3T2e_83hp_Q90cIPam-hwRafdRMDtvajDxDlDp-3ItJ7ml_lInKst2zaFDQEZvvyZAQ/s72-w512-c-h640/IMG_20210129_083558_436.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/01/beki-mpya-yanganitafanya-makubwa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/01/beki-mpya-yanganitafanya-makubwa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy