Mshambuliaji wa klabu ya Yanga pamooja na timu ya Taifa ya Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa, amewawaaga sambamba na kuwashukuru mashabiki...
Mshambuliaji wa klabu ya Yanga pamooja na timu ya Taifa ya Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa, amewawaaga sambamba na kuwashukuru mashabiki wake pamoja na timu nzima kwa muda wote waliokaa pamoja.
Nyota huyo ambaye wikendi iliyopita aliisaidia timu yake kupata ushindi wa bao 5-1 dhidi ya Platinum FC ya Zimbabwe kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, huku yeye akifunga mabao mawili, ameandika maneno yanayo ashiria kuondoka kunako klabu hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram.
“Kwaheri Yanga, Nakupenda, Nashukuru kwa kilakitu” Ameandika Ngassa kupitia kwenye
Ukurasa wake wa Instagram.
Maneno hayo ya Ngassa, Yanahusishwa na matukio ya Juzi katika mchezo dhidi ya Platinum FC, Nyota huyo alipofunga hakushangilia sana kama ambavyo huwa anashangilia siku zote akiwa na furaha, Lakini alionyesha kukunja mikono miwili na kuiweka kifuani ishara ya kuomba msamaha, na pengine akinyanyua mikono juu na chini kuashiria anatoa shukrani na baadaye akaonyesha ishara ya kulia akiweka mkono wake wa kushoto usoni.
Ngassa aliposti picha yake ya juzi akishangilia kwa kulia ambapo aliambatanisha na maneno hayo, kitu ambacho kinaonyesha Yupo njiani kuondoka Yanga.
Kwa muda mrefu sasa Nyota huyo ambaye amewahi kuzichezea timu za Kagera Sugar, Azam FC pamoja na Simba SC, amekuwa hana furaha ya kutosha Jangwani hapo licha ya kuficha ukweli, lakini kwa watu wanao mjua vizuri Ngassa ambaye hadi El Merreikh walikuwa wakitaka huduma yake watakuwa wanakubariana na hili, kwamba hanafuraha licha ya kufunga mabao.
Share na Mwenzako hapo chini
COMMENTS