Wanawake wanaochelewa kubeba ujauzito waonywa
HomeHabariKitaifa

Wanawake wanaochelewa kubeba ujauzito waonywa

  Dk Ali Mzige WANAWAKE wanaochelewa kubeba ujauzito, wameonywa kuwa kuchelewa huko kunawaweka hatarini kuja kupata wa...

Escrow yauma vigogo BoT, TRA
Bocco aenda Algeria kujaribu bahati yake
‘Hatuna kiongozi wa mfano’



 














Dk Ali Mzige

WANAWAKE wanaochelewa kubeba ujauzito, wameonywa kuwa kuchelewa huko kunawaweka hatarini kuja kupata watoto wenye mtindio wa ubongo.
Mbali na hilo, pia wanaume wanaotafuta watoto wakiwa katika umri mkubwa wa zaidi ya miaka 60, nao wametajwa kuwa hatarini kupata watoto wa aina hiyo na wakiepuka hilo, watakosa uwezo mzuri wa akili darasani.
Taarifa ya daktari mkongwe nchini, Dk Ali Mzige aliyotoa wiki hii, amebainisha kuwa hali ya umri mkubwa wa wazazi wa kike na kiume, ndio chanzo kikubwa cha kuzaliwa kwa watoto wa aina hiyo, na siyo uchawi wala mazingaombwe.
“Naomba niweke wazi kwamba, mama mwenye umri zaidi ya miaka 35 kama ndio anaanza kuzaa kwa mara ya kwanza, Mungu aepushie mbali, lakini ana uwezekano mkubwa wa kupata mtoto mwenye mtindio wa ubongo. “Mbali na hayo, pia kwa baba mwenye umri mkubwa miaka zaidi ya 60 na ushei, akitaka kutafuta mtoto uwezekano upo wa kupata mtoto mwenye mtindio wa ubongo. Kwa hiyo ushauri wangu kwa wazee wenzangu tunaostaafu sasa, tulee wajukuu tusianze tena kutotoa vifaranga,” ameeleza Dk Mzige katika taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa Dk Mzige, kisayansi umri mzuri wa kuoa au kuolewa na kuzaa kupata watoto wenye afya nzuri, ni kati ya miaka 18 na 35 kwa pande zote mbili baba na mama.
Changamoto kijamii
Akizungumzia changamoto wanazokabiliana nazo watoto hao, Dk Mzige alisema ni pamoja na unyanyapaa kutoka katika jamii kwa watoto hao pamoja na wazazi wa waliowazaa.
Amesema kutokujua chimbuko la mtindio wa ubongo katika jamii, kumekuwa kukihusishwa na imani za kishirikina, kwamba mzazi amefanya kila awezalo, ili mwanawe awe na mtindio wa ubongo, ili apate mali na kutajirika.
Mbali na wazazi kuonekana kusababisha mtoto wao kuwa na hali hiyo kishirikina, Dk Mzige alisema watoto hao pia wamekuwa wakitengwa na jamii na wakikua hasa wanawake, hudhalilishwa kijinsia ikiwemo kubakwa.
“Wengi hunajisiwa na kubakwa na watu wenye akili timamu, kwa imani kuwa kufanya tendo hilo na mtu mwenye ulemavu, utapata utajiri na mafanikio mazuri katika shughuli zako,” alisema.
Changamoto kiakili Alisema wanaozaliwa wakiwa na mtindio wa ubongo, huchelewa kukua kiakili na kimaumbile, ni wapole sana hawana fujo kama watoto wengine wanaozaliwa kikamilifu.
Pia huchelewa kutambaa, kunyanyuka, kuzungumza na wanakuwa na misuli ambayo ni dhaifu haina nguvu ya kusukuma na kupiga mateke kama watoto wengine.
“Uelewa wao kiakili uko katika asilimia 50 (IQ), ukilinganishwa na watoto wa kawaida ambao wana uelewa na ufahamu wa asilima 100,” alisema Dk Mzige.
Dk Mzige pia alifafanua kuwa kama baba atakuwa na umri wa zaidi ya miaka 60, kama mtoto hatazaliwa na mtindio wa ubongo, mtoto huyo kiakili atakuwa na kasoro endapo umri wa baba utakuwa umesogea na yeye bado anaendelea kupata watoto.
Aidha wanaozaliwa na tatizo hilo, magonjwa makuu yanayosababisha vifo kwao ni saratani ya damu (leukemia) na magonjwa ya moyo na wengi hawafikishi umri wa kuishi wa miaka 40.
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Wanawake wanaochelewa kubeba ujauzito waonywa
Wanawake wanaochelewa kubeba ujauzito waonywa
http://habarileo.co.tz/images/mzige-again.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2014/12/wanawake-wanaochelewa-kubeba-ujauzito.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2014/12/wanawake-wanaochelewa-kubeba-ujauzito.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy