Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ambaye ni Katibu Mwenezi wa Chama cha NCCR-Mageuzi, amesema hana sababu yoyote ya kuhama chama c...
Mbunge
wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ambaye ni Katibu Mwenezi wa Chama cha
NCCR-Mageuzi, amesema hana sababu yoyote ya kuhama chama chake na
kujiunga na chama kipya cha siasa cha Alliance for Change and
Transparency (ACT-Tanzania).
Kafulila
alisema hayo jana alipokuwa akijibu swali kuhusu kusambaa kwa tetesi
katika mitandao ya kijamii kwamba, anahamia chama hicho akiambatana na
aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe aliyehamia chama hicho
hivi karibuni.
“Tetesi
hizo zinatokana na tabia yangu ya kuwa na marafiki wengi katika chama
hicho kipya, lakini nashangaa nina marafiki wengi CCM na hata Chadema,
lakini hawasemi nahamia vyama hivyo ila ACT. Hizo ni tetesi tu sina
sababu ya kuhama chama changu,”alisema.
Alisema
Zitto alihama Chadema kutokana na mgogoro uliokuwepo baina yake na
Chadema, hivyo alikuwa na sababu ila yeye akihama bila kuwa na sababu,
itakuwa haina maana.
Alisema
yeye bado ni Katibu Mwenezi wa NCCR-Mageuzi na anaendelea na kampeni za
kujenga chama hicho ikiwemo yeye kurudi bungeni pamoja na chama hicho
kuongeza wabunge wengi zaidi.
COMMENTS