Msemaji Mkuu Wa Serikali Aipongeza Ncaa Kwa Uhifadhi Wa Ngorongoro
HomeHabari

Msemaji Mkuu Wa Serikali Aipongeza Ncaa Kwa Uhifadhi Wa Ngorongoro

Na Mwandishi wetu, NCAA. Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari maelezo Bw. Gerson Msigwa amepongeza uongozi wa Maml...


Na Mwandishi wetu, NCAA.

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari maelezo Bw. Gerson Msigwa amepongeza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro kwa jitihada za uhifadhi wa eneo la Hifadhi ya Ngorongoro hali inayovutia watalii wa ndani na nje ya Nchi kutembelea eneo hilo.

Msigwa ametoa kauli hiyo jana wakati wa ziara ya kikazi kutembelea eneo la hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kijifunza shughuli mbalimbali za Uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii.

“Nimefurahi kutembelea eneo la Ngorongoro na kuona nchi yetu ilivyobarikiwa kuwa na rasilimali hii muhimu, naipongeza NCAA kwa kazi kubwa ya kuhifadhi vivutio vya eneo hili, naamini uhifadhi endelevu ndio uliosaidia kutunza mvuto na muonekano wa bonde hili ambalo ni muhimu kwa wageni wa ndani na nje ya nchi wanaotembelea Ngorongoro na ikolojia nzima ya kuelekea Hifadhi ya Serengeti.”

Msigwa ameongeza kuwa uhifadhi wa eneo la Ngorongoro ni muhimu kwa kuwa ni moja kati ya maajabu saba ya bara la Afrika na ni eneo lenye historia ya chimbuko la binadadamu wa kale, ugunduzi wa nyayo za binadamu na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa kuunga mkono juhudi za serikali kulitangaza ili kuendelea kuwa kimbilio la wageni wengi ambao mchango wao unaongeza Mapato ya Serikali.

Amebainisha kuwa pamoja na mtikisiko wa ugonjwa wa Uviko-19 jitihada za Serikali na wadau mbalimbali zimewezesha idadi ya wageni wanaotembelea Tanzania kuendelea kuongezeka na kufikia wastani wa wageni Milioni 1.7 kwa mwaka.

“Idadi ya watalii wa ndani pia imezidi kuongezeka, tuendelee kuongeza juhudi za kutangaza vivutio vyetu, naamini ongezeko la watalii wa ndani ni hamasha na chachu ya watalii wa nje kuja, kadri tunavyoongeza mapato yatokanayo na utalii tunazidi kuisaidia Serikali kuboresha huduma muhimu kama afya, maji, shule na uboreshaji wa miundombinu ya utalii”

Katika eneo la Bonde la Ngorongoro Msigwa amefurahishwa na uwepo wa Wanyama wa aina mbalimbali wakiwemo Wanyama maarufu watano (Big Five). “Nimeona wanyama mbalimbali wakiwemo wote the big five na wengine wengi kwa muda usiozidi saa 2. Nimeamini usemi wa _Ngorongoro


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Msemaji Mkuu Wa Serikali Aipongeza Ncaa Kwa Uhifadhi Wa Ngorongoro
Msemaji Mkuu Wa Serikali Aipongeza Ncaa Kwa Uhifadhi Wa Ngorongoro
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhoXzTLHYb8eps7IvKF3qc_V3Ee8w4E85H-Q8AqpZERT8L_Zemk5CdougEEHJKXm9wuzqggX91Pxwj9L9U_7UMB0paPNNbwsNYJrj3St6QLhgRfWg02nRgczcGu1D_48jICPq6lxUWBcHkjT6jmlWCaHI4dHZQ_Mu1_n2lJlpnFmYiVVkVUNr2WpcMBKg/s16000/1.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhoXzTLHYb8eps7IvKF3qc_V3Ee8w4E85H-Q8AqpZERT8L_Zemk5CdougEEHJKXm9wuzqggX91Pxwj9L9U_7UMB0paPNNbwsNYJrj3St6QLhgRfWg02nRgczcGu1D_48jICPq6lxUWBcHkjT6jmlWCaHI4dHZQ_Mu1_n2lJlpnFmYiVVkVUNr2WpcMBKg/s72-c/1.png
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/03/msemaji-mkuu-wa-serikali-aipongeza-ncaa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/03/msemaji-mkuu-wa-serikali-aipongeza-ncaa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy