Mshambuliaji Javier Hernadez ” “Chicharito” amesema kuendelea kukaa benchi katika klabu ya Real Madrid kunamfanya akose furaha...
Mshambuliaji Javier Hernadez ”
“Chicharito” amesema kuendelea kukaa benchi katika klabu ya Real Madrid
kunamfanya akose furaha na kukosa kujiamini.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa
Mexico alijiunga na mabingwa hao wa Ulaya mwanzoni mwa msimu huu
akitokea katika klabu ya Manchester United kwa mkataba wa mkopo wa mwaka
mzima.
Katika mkataba huo Real Madrid
wanakipengele cha kumsajili moja kwa moja mshambuliaji huyo lakini hana
uhakika kama ataendelea kubaki klabuni hapo. “Ninajitahidi kwa asilimia
100 kwenye mazoezi lakini kwenye mechi sichezi,hilo linaondoa kujiamini
na ninakosa furaha” alisema Chicharito
Tangu ajiunge na Real Madrid
Chicharito amecheza mechi 13 za La Liga na kufanikiwa kufunga magoli
matatu na kutoa pasi ya mwisho moja.
Chicharito,26, alijiunga na Real
Madrid mara baada ya kukosa namba katika kikosi cha Louis Van Gaal na
pia kuwasili kwa mshabuliaji Radamel Falcao kulichangia kwa kiasi
kikubwa.
Mchezaji huyo ambaye mkataba wake
katika klabu ya Manchester United unaisha June 2016 alifunga katika
mechi ya kirafiki ya juzi jumamosi ambayo ilimalizika kwa Mexico
kushinda 1-0 dhidi ya Ecuardo.
COMMENTS