Inauma sana! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kusikia habari hii kuwa ile ofisi ya aliyekuwa mwigizaji kinara wa sinema za Kibo...
Ofisi ya Kampuni ya Kanumba The Great Films illiyopo Sinza Moriijini Dar imefungwa rasmi huku vitu vikihamishwa usiku.
Tukio
hilo la kusikitisha lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri
Februari 2, mwaka huu, majira ya saa 1:30 usiku baada ya kutonywa na
jirani mmoja anayefanya biashara zake karibu na ofisi hiyo.
Shuhuda huyo alidai kwamba mtekelezaji wa zoezi hilo ni mmoja wa watoto wa Mama Kanumba, Flora Mtegoa (jina halikupatikana mara moja) ambaye aliamua kufanya shughuli hiyo usiku ili kukwepa kuonekana.
Shuhuda huyo alidai kwamba mtekelezaji wa zoezi hilo ni mmoja wa watoto wa Mama Kanumba, Flora Mtegoa (jina halikupatikana mara moja) ambaye aliamua kufanya shughuli hiyo usiku ili kukwepa kuonekana.
“Ninyi
Global mnapitwa, mtoto wa Mama Kanumba anahamisha vitu ofisini kwa
Kanumba, tayari zoezi limeanza,” alisema jirani huyo aliyeomba hifadhi
ya jina na kuongeza kuwa ofisi hizo zinahamishwa mahali hapo kwa sababu
kodi ya jengo hilo imeongezeka kutoka laki mbili za awali na kuwa laki
sita kwa mwezi, gharama ambayo inatajwa kumshinda mama huyo.
Wanahabari
wetu walifika eneo la tukio ndani ya dakika sifuri ambapo walishuhudia
gari aina ya Toyota Canter likiwa limepaki nje ya ofisi hiyo huku watu
wanaodaiwa kuwa ni wabeba mizigo wakiingia na kutoka ndani ya ofisi
hiyo wakiwa na vitu mbalimbali kisha kuviingiza kwenye gari hilo.
Kwa
ustadi mkubwa, mapaparazi wetu waliopiga kambi katika eneo hilo
walishuhudia masanduku ya vioo yaliyokuwa yakitumika kuwekea CD na DVD
za marehemu Kanumba yakipandishwa kwenye gari hilo.
Baada ya zoezi hilo kushika kasi, wanahabari wetu walizama ndani na kujionea hali halisi ambapo walishuhudia chumba kikiwa wazi huku picha za ukutani zikiwa zimeshushwa na kuwekwa pamoja na vitu vingine tayari kwa kupandisha kwenye gari.

Hata
hivyo, mtu aliyetajwa kuwa mmoja wa watoto wa Mama Kanumba aliwazuia
mapaparazi wetu kupiga picha za ndani ya chumba hicho na kujifungia
mlango kwa ndani huku wakisitisha zoezi la kupakiza vitu kwenye gari kwa
muda wakiwataka mapaparazi waondoke eneo hilo.
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wabeba mizigo hao alisema kuwa, walifika eneo hilo na gari lao kwa ajili ya kuhamisha mizigo kutoka ndani ya ofisi hiyo na kuongeza kuwa yeye hakufahamu chochote zaidi ya mhusika mwenyewe ambaye ni mtoto wa Mama Kanumba.

Mama
Kanumba alipopigiwa simu na mwandishi wetu alikiri kupandishwa kwa kodi
ya ofisi hiyo kwa kiasi kikubwa na kudai kuwa alishindwa kulipa fedha
hizo kwa kuwa hapati faida yoyote kutokana na ofisi hiyo zaidi ya
hasara.
“Kwa
kweli kodi imekuwa kubwa mno, siwezi kulipa maana tangu mwanangu
afariki dunia (Aprili 7, 2012) siku hadi siku kodi imekuwa ikizidi.
“Kipindi
Kanumba anafariki dunia kodi ilikuwa laki mbili kwa mwezi, tangu hapo
imekuwa ikipanda mara kwa mara mpaka sasa ni laki sita kwa mwezi na
wanataka nilipe yote ya mwaka mzima, kusema kweli nimeshindwa.
“Hakuna
kikubwa ninachonufaika na kampuni kiasi cha kulipa fedha nyingi kiasi
hicho japo nimefanikiwa kutoa filamu mbili tu mpaka sasa.
“Nimeamua kuachana nayo (ofisi) nitafakari sehemu nyingine ya kuendeleza kampuni,” alisema Mama Kanumba.
“Nimeamua kuachana nayo (ofisi) nitafakari sehemu nyingine ya kuendeleza kampuni,” alisema Mama Kanumba.
Kufungwa
kwa ofisi ya Kanumba kunakuja ikiwa ni siku chache baada ya kuibuka kwa
skendo kuwa ilikuwa imegeuzwa kichaka cha ufuska na baadhi ya wasanii
na machangudoa ambao usiku huonekana nje ya ofisi hiyo na wateja wao.
Hadi sasa haifahamiki kama ndiyo mwisho wa Kanumba The Great Films au itafunguliwa sehemu nyingine au ndiyo imekufa moja kwa moja japokuwa kuna taarifa kuwa mara baada ya ofisi ya Kanumba kufungwa, kwa sasa ofisi hiyo ina mpangaji mpya.

COMMENTS