Mwigizaji wa filamu nchini Wema Sepetu ‘Wema’, amemfungulia kesi ya madai mpenzi wake wa zamani ambaye ni mwanamuziki wa bongo flev...
Kwa mujibu wa mtandao wa Shirika la Utangazaji (BBC) idhaa ya Kiswahili, Wema aliripoti madai yake kituo cha Polisi Oysterbay akidai kuwa alimpatia mwanamuziki huyo kiasi hicho kwa makubaliano ya kazi na kuahidi kumlipa, lakini amekwenda kinyume makubaliano yao.
Muhusika
mkuu ambaye ni Wema alitoa maelezo kwamba watu wanamtupia lawama
kutokana na hatua aliyofikia, lakini amedai kuwa amelazimika kufanya
hivyo kwa kuwa yeye ndiye aliyeingia dhamana na taasisi Focus Vicoba
kuchukua fedha hizo.
“Naona
watu wengi wananilaumu kwa kuwa nimemfungulia kesi Diamond, pasipo
kuelewa kama fedha hizo pia hazikua zangu bali ni mkopo ambao niliingia
dhamana katika taasisi ya utoaji mikopo ya Vicoba.
“Kupitia mfuko wa
Focus Vicoba nilichukua mkopo huo kwa lengo la kumpatia Diamond, ili
aweze kuandaa miradi yake tena kwa makubaliano kuwa atazirudisha ili
tuweze kufanya marejesho ya mkopo tuliochukua,” alisema Wema.
Mrembo huyo alieleza muda waliiopeana ahadi ya kurudisha fedha hizo umepita na Diamond haoneshi dalili ya kuzirejesha wakati wanatakiwa kuzirudisha kwa wakati .
“Yote haya yasingenikuta, lakini sina jinsi kwani natakiwa kurudisha pesa za watu nimekuwa nikimpigia simu Diamond hataki kupokea simu zangu, lakini kama alitaka kunidhulumu ni bora angejiunga mwenyewe na hawa Vicoba ili apate mkopo na kufanya mambo yake au kama aliona hawezi kwa kujishtukia basi angetumia ile tovuti yao, angepata kwa urahisi na hakuna mtu yeyote angejua kama amekopa ila sio kukimbia kulipa deni la watu,” alisema.

Wema
ambae alimwekea dhamana, yupo katika kipindi kigumu ambacho kinaweza
kupelekea kufilisiwa mali zake ambazo aliziandikisha wakati wa kuchukua
mkopo huo ili ziweze kufidia deni hilo.
Kwa
mujibu wa kiongozi wa taasisi hiyo ambae aligoma kutajwa jina lake
gazetini, alisema kuwa ni kweli Wema alifika katika ofisi zao zilizopo
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, ili apewe muongozo lakini alipotakiwa
kufuata taratibu za kiofisi kama wanachama wengine wanavyofanya katika
vikundi, hakukubaliana na utaratibu, hivyo kushauriwa ajiunge kupitia
tovuti .
Alipotafutwa
Meneja wa Wema, Martin Kadinda, kuzungumzia swala hili alisema
hajui chochote kuhusu kufungulia kwa kesi hiyo, akaomba apewe muda
kumtafuta msanii huyo ili aweze kupata ufafanuzi juu ya suala hilo,
lakini hakueleza nini kilichojiri na kusisitiza asubiriwe.
Pia
alipotafutwa meneja wa Diamond, Babu Tale, kuzungumzia swala hili
alionekana kushtushwa na habari hizo na kudai kuwa hazina ukweli
wowote.
Chanzo: Gazeti la Mtanzania
Chanzo: Gazeti la Mtanzania
Chanzo Bongomovies
COMMENTS