Na. Richard Bakana Simba SC imejikuta ikipigishwa kwata la nguvu na wanajeshi wa Mgambo Shooting katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga baada ya...
Na. Richard Bakana
Simba SC imejikuta ikipigishwa kwata la nguvu na wanajeshi wa Mgambo Shooting katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga baada ya kupokea kipigo cha bao 2-0, Huku mlinda mlango wake namba moja Ivo Mapunda akizawadiwa kadi Nyeku.
Mabao ya Mgambo Shooting yamefungwa na Ally Idd kunako dakika ya 44 kwa shuti kali ambalo Ivo Mapunda alishindwa nini afanye nakuwawezesha wenyeji hao kureje katika vyumba vya kubadirishia Nguo wakiwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili timu zote zikisaka bao, Huku Mgambo wakionekana kuwa juu zaidi ya Simba kwa kushambulia zaidi lango la Mnyama, Wanajeshi hao walijikuta wakizawadiwa penati baada ya kipa wa Simba Ivo Mapunda kumfanyia madhambi Mshambuliaji ambaye alikuwa anaelekea kufunga bao kitu kilicho sababisha Kipa huyo apewe kadi Nyekundu na Mgambo kuzawadiwa penati.
Mgambo walijiandikia bao la pili na laushindi kupitia kwa Maganga dakika ya 67 baada ya kupiga penati hiyo na kumfunga Peter Manyika.
COMMENTS