Picha ya Maktaba: Wanamgambo wa moja ya vikundi vya kislam huko Mali. Watu watano wameuwawa baada ya watu wenye bunduki wan...
Watu watano wameuwawa baada ya watu wenye bunduki wanaoaminika kuwa
wapiganaji wa Al-Qaida kushambulia kituo cha kijeshi kilichoko katikati
ya Mali.
Tukio hilo limefanyika usiku wa kuamkia Jumatatu kwenye mji wa Nampala ulioko kilomita 530 kaskazini mwa mji mku wa Mali, Bamako, karibu na mpaka wa Mauritania.
Afisa mmoja kutoka Nampala ameiambia Sauti ya America (VOA) kwamba wanajeshi watatu wa Mali, pamoja na wapiganaji wawili wameuwawa kwenye mapigano hayo.
Hakuna aliyetangaza kuhusika na mauaji hayo lakini kundi la Al-Qaida, linashukiwa kuhusika na limekita mizizi katika eneo hilo.
Kundi la Al Qaida lililoko ukanda wa Islamic Magreb, pamoja na vikundi vingine vilijtwalia sehemu kubwa ya kaskazini mwa Mali, mwaka 2012 kabla ya kuondolewa na wanajeshi walokuwa wakiongozwa na Ufaransa.

COMMENTS