Ghasia za Burundi Waandamanaji wanaompinga rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu wameagi...
Ghasia za Burundi
Waandamanaji
wanaompinga rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu
wameagiza kusitishwa kwa maandamano hayo kwa siku mbili.
Msemaji wa vyama vya kiraia amesema kuwa hatua hiyo itazipa fursa familia za wale waliouawa katika maandamano hayo kuomboleza.Takriban watu sita wamefariki tangu maandamano hayo yaanze jumapili iliopita.
Awali rais wa taifa hilo aliwaonya maafisa wa vyama vya kiraia kwamba ataawadhibu.
Wapinzani wamemshtumu kwa kukiuka katiba.
Chanzo BBC
COMMENTS