Augustine Mrema MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema ame...
Akizungumza katika mkutano wa Kamati Kuu uliofanyika kwenye Makao Makuu ya chama hicho, Dar es Salaam jana, alisema hawezi kujiuzulu hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika.
Mrema anatuhumiwa na wanachama wa chama hicho kwamba anaongoza kidikteta, kinyume na katiba ya chama pamoja na kuongoza kikabila.
Alisema kwamba makundi ya watu wanaojiita wanachama wa chama hicho waliokwenda kutoa malalamiko yao kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, hayatambui na kwamba ni wahuni.
Mbunge huyo wa Vunjo, alisema kwamba makundi hayo ya vijana huwa wanajitokeza wakati wa uchaguzi ili kuchochea fujo katika chama hicho.
“Lazima tuwapige vita vijana hawa wanaojitokeza wakati wa harakati za uchaguzi. Mimi naweza kulifananisha kundi hilo na lile la al Shabaab kwani hatuwatambui kikatiba,’’alisema Mrema.
Pia aliongeza kuwa katika chama hicho anaongoza kupitia katiba ya chama na ya nchi hivyo tuhuma hizo dhidi yake hazina nafasi kwa wakati huu.
COMMENTS