Ommy Dimpoz akizungumza mbele ya wanafunzi wa Mbezi High School walipofika hapo na Idris kuwapa moyo na kutoa sh...
MSANII wa
Bongo Fleva, Ommy Dimpoz na mshindi wa Big Brother 2014, Idris Sultan,
mapema leo walifanya tukio la kipekee baada ya kutinga katika shule ya
Mbezi High School, waliosoma na kuwashitukiza walimu na wanafunzi kwa
pamoja kabla hawajaingia kwenye vipindi vya masomo.
Wakizungumza
katika ishu hiyo, Ommy Dmpoz na Idris walisema walikutana na kukaa
pamoja na kujadiliana juu ya kwenda shuleni hapo kuwapa moyo na
shukurani kwa ujumla walimu na wanafunzi wa shule hiyo ambayo walisoma.
“Tumekaa
na tukapanga hili wazo ili tuweze kuwashukuru kwa yote mnayotutendea,
hususani kufuatia ushindi wangu wa Big Brother, ambao naamini kabisa kwa
vyovyote mchango wenu ulikuwa mkubwa kwangu. Mwenzangu Ommy Dimpoz
alitangulia kumaliza shule kabla yangu, ila mmekuwa mkimsapoti kwa kila
anachokifanya kwenye muziki wake,” alisema Idris.
COMMENTS