Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Haruna Niyonzima Nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda Haruna Niyonzima ameitwa kwenye kikosi cha wach...
Mchezaji huyu anacheza mpira wa kulipwa kwenye klabu ya Yanga lakini hakuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda kilichopambana dhidi ya Morocco mwezi wa kumi na moja mwaka jana baada ya kocha mkuu wa kikosi hicho Stephen Constantine kusema yuko kwenye maandalizi ya kuandaa timu itakayoshiriki fainali za (Chan) mwaka ujao.
Mwaka ujao nchi ya Rwanda itakuwa mwenyeji wa mashindano ya soka ya bara la Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.
Wachezaji walioitwa kuunda kikosi hicho ni:
Walinda mlango: Marcel Nzarora (Police), Olivier Kwizera (APR) and Steven Ntalibi (Police)
Mabeki:
Soter Kayumba (AS Kigali), Ismail Nshutiyamagara (APR), Emery Bayisenge (APR), Michel Rusheshangoga (APR), Fitina Ombelenga (SC Kiyovu), Janvier Mutijima (AS Kigali) and Eric Rutanga (APR).
Viungo:
Haruna Niyonzima (Yanga), Jean Baptiste Mugiraneza (APR), Rachid Kalisa (Police), Justin Mico (AS Kigali), Savio Nshuti Dominique (Isonga), Patrick Sibomana (APR), Jean Claude Zagabe (Mukura), Kevin Muhire (Isonga), Andrew Buteera (APR) and Emmanuel Sebanani (Police).
Washambuliaji:
Ernest Sugira (AS Kigali), Danny Usengimana (Isonga), Bertrand Iradukunda (APR), Innocent Ndizeye (Amagaju) and Issa Bigirimana (APR).
Wengine ni:
Ismail Nshutiyamagara (APR), Haruna Niyonzima (Young Africans/Tanzania), Jean Baptiste Mugiraneza (APR), Jean Claude Zagabe (Mukura), Ernest Sugira (AS Kigali).
COMMENTS