Katibu feki wa Ikulu akamatwa
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
HomeHabariKitaifa

Katibu feki wa Ikulu akamatwa

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linamshikilia mkazi ...


JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linamshikilia mkazi wa Mbagala Rangi Tatu, Haroub Mtopa (44) kwa kujifanya mtumishi wa umma kupitia cheo cha Katibu wa Rais, Jakaya Kikwete, Prosper Mbena.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi jioni.

Kova alisema Mtopa alikuwa na mazoea ya kujifanya mtumishi wa Ikulu kwa nia ya kudanganya watu kwamba anaweza kuwasaidia shida zao ili ajipatie fedha.

Katika kufanya kazi zake za kitapeli, Kova alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akiingia na kutoka Ikulu mara kwa mara, huku akijifanya kuwa na shida nyingi hivyo alikuwa akiomba msaada.

‘’Huyu mtu ni tapeli wa muda mrefu sana, tulimkamata baada ya mwananchi mmoja kuzungumza na mtuhumiwa huyo na kuahidiana kumpa Sh 500,000 na kutanguliziwa Sh 250,000.

Baadae aliitwa siku nyingine afuate fedha iliyobaki. ‘’Mwananchi huyo ambaye hakumtaja jina, alimhofia Mtopa ndipo alipotoa taarifa Polisi kisha akamwambia mtuhumiwa huyo aende kuchukua fedha iliyobaki, hatua iliyosaidia Polisi kumkamata kwa urahisi,’’ alisema.

Kova alisema kuwa mtu huyo ni hatari kwa sababu kutumia cheo cha Katibu wa Rais wakati inamaanisha kwamba mtu huyo aliweza kutapeli watu wengi sana kupitia cheo hicho.

Kwa mujibu wa Kova, mtuhumiwa huyo amekuwa akizunguka katika wizara mbalimbali ikiwamo ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Maji na taasisi nyingine zinazotoa huduma kwa jamii, kwa lengo la kuomba msaada.

Alisema kabla ya kumkamata, walishirikiana na Ikulu baada ya watu wengi kupeleka malalamiko yao kuhusu mtuhumiwa huyo.

Kova aliwaasa wananchi kuepuka kujifanya watumishi wa umma kwani ni kosa kisheria na kuongeza kuwa wameweka kikosi maalumu kitakachoshughulikia masuala ya watu wanaozunguka zunguka nje za ofisi za watu pasipo shughuli maalumu.
 
Chanzo Habari Leo
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Katibu feki wa Ikulu akamatwa
Katibu feki wa Ikulu akamatwa
http://habarileo.co.tz/images/resized/images/kamanda-suleiman-kova_300_172.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/03/katibu-feki-wa-ikulu-akamatwa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/03/katibu-feki-wa-ikulu-akamatwa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy