Rais Mugabe Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa umoja wa Afrika Au kwenye mkutano unao...
Rais Mugabe
Rais
wa Zimbabwe Robert Mugabe, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa umoja
wa Afrika Au kwenye mkutano unaoendelea mjini Addis Ababa Ethiopia
Wajumbe
walimteuwa Rais Mugabe mwenye umri wa miaka tisini kwa kauli moja
katika mkutano huo na kumtakia mema kwenye harakati mbalimbali za
kuimarisha uchumi wa bara la Afrika.
Mugabe amechukua nafasi hiyo ya Uenyekiti kuziba nafasi inayoachwa na Rais wa Afrika Kusini Nkosazana Dlamini-Zuma.
Wadadisi
wa masuala ya kisiasa wametilia shaka uteuzi huo wa Rais Mugabe
kuongoza Zaidi ya nchi arobaini ambazi ni wanachama wa umoja huo
wakieleza kuwa Mwenyekiti huyo mpya hana mahusiano mazuri mataifa ya
Magharibi
Shaka
hiyo dhidi ya Mugabe pia imejadiliwa na wanasiasa kuwa pengine ikiwa
chachu ya maendeleo kwa Afrika kwa kujitawala yenyewe bila kutegemea
nchi wafadhili.
COMMENTS