Aliyekuwa mlinzi binafsi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. WILBROAD SLAA kwa...
Aliyekuwa
mlinzi binafsi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Dk. WILBROAD SLAA kwa jina la Khalid Kangezi leo ameibuka na
kukanusha taarifa zilizotolea na chama chake kuwa alikuwa anakula njama
za kumuua katibu mkuu huyo na kusema kuwa amefanyiwa hujuma za wazi
ndani ya chama hicho.
Akizungumza
kwa uchungu ndani ya ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es Salaam
mbele ya wanahabari leo, amesema kuwa kilichotokea hakijui ila
anashangaa kuwa chama kimeamua kumtenda na kumpiga sana wakimtuhumu
kutaka kumuua kiongozi huyo jambo ambalo amesema kuwa ni la kushangaza
na halina ukweli wowote ule.
Amesema
kutokuelewana kwake na Katibu Mkuu wa chama hicho kulianza pale
alipoanza kupishana kwa maneno kati yake na mke wa Dk. Slaa ambapo Slaa
alimuamuru aende kwa mke wake akamalize ugomvi wake na mke wake ndipo
aendelee na kazi jambo ambalo amesema kuwa alishangaa kuwa hakuwa na
ugomvi na mke wa Dk. Slaa na hakuweza kufanya hivyo.
Amesema
kuwa siku ya Jumamosi aliitwa Makao Makuu ya chama kwa mualiko kuwa
kuna kikao maalum na mwenyekiti wa chama hicho na alipofika aliingizwa
chumbani ambapo aliwakuta vijana watano wa chama hicho ambao amewataja
kwa majina na bila kumjuza kitu chochote walianza kumpiga mateke,
kumtesa, kumvua nguo, kumwagia maji huku wakimtuhumu kuwa amepewa sumu
na viongozi wa chama cha CCM ili amuue katibu mkuu dk. Slaa.
“Jamani
hivi inaingia akilini kweli mimi leo na maisha yangu haya niwe na
uhusiano na watu wa usalama na CCM,huu ni uwongo wa hali ya juu na
wanataka kunichafua kwa jamii, tena niseme ukweli chama hiki kinataka
kuficha ukweli juu ya mambo waliyonitendea.”
“Ni
kwamba mimi nimekuwa mlinzi wa Slaa kwa muda wa miaka mingi sana, tena
mimi nilikuwa nampikia na kumtengea hadi chai ya kunywa eti leo niambiwe
naandaa mipango ya kumuua huo ni unafiki” amesema Kagenzi
Katika
Jambo la kushangaza Mlinzi huyo amefichua mipango ya kitesaji na
kigaidi inayofanya na CHADEMA huku akisema wameandaa ofisi ya utesaji.
“Jamani
hiki chama ambacho kina ndoto ya kuchukua nchi leo kinaandaa mipango ya
mauaji na utesaji kama walivyonifanyia? Maana wameniteka na kunifungia
kwenye chumba cha utesaji wanachomiliki wao wamechoma visu na kuweka
kwenye Mashine ya umeme bila kosa lolote, eti wakinishinikiza mimi
nitaje wanaonituma, jamani nawaambia mimi hanitumi mtu” ameedelea kusema
Kagenzi.
Aidha, Kagenzi amekitupia lawama chama hicho huku akisema kwenye mateso waliyomtesa yamemfanya apoteze hata nguvu za kiume .
Alibanisha
kuwa hata alivyokuwa mlinzi wa Dokta Slaa kwa miaka mitano zaidi
alikuwa analipwa malipo madogo ya Laki tatu kwa mwezi lakini anasema
kuwa hakuandaa mipango ya yoyote ya kumuua,lakini anashangaa kwanini leo
wanamsingizia kiasi hicho kwani amedai kuwa kama angekuwa anataka
kufanya vitendo vya kukisaliti chama angefanya huko nyuma.
Kuhusu kuingiziwa Milioni saba kwenye simu yake na watu wa Usalama wa Taifa
Kagenzi amesema hizo ni taarifa za uongo zinazosemwa kwani hata simu yake haina salio ya pesa na haijawahi kupokea pesa hizo.
Hatua atakazochukua
Kagenzi
amesema hatua iliyobaki sasa hivi ni kwamba tayari ameshahojiwa na
jeshi la Polisi na kilichobaki sahivi ni kusubiri kesi mahakamani ili
kukishtaki chama hicho kwa Vitendo walivomfanyia navyodai ni vya kiuaji.
COMMENTS