AIBU ILIYOJE: MKE AVAA KININJA, AMFUATILIA MUMEWE, AMFUMANIA
HomeMatukio

AIBU ILIYOJE: MKE AVAA KININJA, AMFUATILIA MUMEWE, AMFUMANIA

Aibu iliyoje! Tukio la aina yake limetokea maeneo ya Diluxe jijini hapa baada ya mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Faudhia almaaruf...

MWANAFUNZI ATEKWA, AUAWA
MCHUNGAJI ANASWA NA WANAWAKE WATATU GESTI WAKILA URODA PATA HABARI YOTE HAPA
Hosteli ya mabibo yaharibika kwa kuungua na moto>>>>>Soma zaidi hapa
Aibu iliyoje! Tukio la aina yake limetokea maeneo ya Diluxe jijini hapa baada ya mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Faudhia almaarufu mama Baraka kumfumania mumewe akisaliti ndoa yao mbichi.
Faudhia akihamaki baada ya kufumaniwa.
Kwa mujibu wa mama Baraka, amekuwa akimfuatilia mumewe kwa muda mrefu baada ya kutonywa na wambeya kuwa baba mtoto wake huyo amekuwa akichepuka na ‘kichenchede’ (mrembo) wa mjini.
Siku ya tukio, hivi karibuni ilidaiwa kwamba mume huyo alirudi nyumbani mapema, akapumzika kidogo, majira ya saa sita mchana aliamka, akaoga na kupewa chakula kama kawaida kisha akamuaga mkewe kuwa anaenda ofisini kuna dharura imetokea ghafla.
...Akiwa anavaa.
Kwa mujibu wa mke huyo, jamaa alipotoka tu naye akachukua pikipiki ambayo ilikuwa tayari imeandaliwa na kuanza kumfuatilia kwa nyuma kila alipokuwa anaenda ambapo alienda katika baa mbalimbali za Villa Park Resort, Kibo na nyingine.
Ilisemekana kwamba, alipofika Diluxe Night Club, alipiga honi kisha akajitokeza kimwana mmoja na kuingia kwenye gari hilo wakaondoka, walipofika kwenye eneo la giza maeneo hayohayo ya Diluxe Night Club, gari lilisimama, wakashuka, wakahamia siti ya nyuma.
OFM WAPIGIWA SIMU
Kamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers na vijana wake, wakiwa katika pikipiki zao ziendazo kasi wakisakanya habari maeneo ya Jiji la Mwanza ghafla walipokea taarifa kutoka kwa chanzo chao kuwa kuna tukio maeneo hayo.
OFM walifika maeneo hayo na kukuta timbwili la nguvu ndani ya gari huku mama mmoja aliyevaa kininja akimwadhibu msichana aliyekuwa nusu utupu na mumewe ndani ya gari.Wakati wa timbwili hilo, mchepuko alivaa suruali na kusahau kuvaa kufuli pakaendelea kuchimbika.
MAMA BARAKA AFUNGUKA
Akizungumza na OFM akiwa eneo la tukio, mama Baraka alisema kuwa alikuwa na kazi kubwa ya kumfuatilia mumewe kwa siku nyingi lakini mumewe huyo alikuwa akipiga chenga.“Nilianza kumfuatilia mume wangu kwa muda mrefu sana baada ya kupata taarifa kuwa huwa ana tabia ya kufanya mapenzi kwenye gari na wanawake.“Nilishamuuliza zaidi ya mara tatu kutaka kujua kama kweli ana tabia hiyo lakini alinikatalia katakata.”


MUME ATAKA KUKATA MSHIKO
Mume huyo alipoulizwa juu ya tabia hiyo alikataa katakata kuongea na kuwambia makamanda wa OFM kuwa hayo mambo anaomba yaishie hapohapo kisha kuzama kwenye waleti na kutoa fedha.
Hata hivyo, makamanda wetu walizikataa na kuendelea kufanya kazi yao kwa mujibu wa kiapo chao cha kutopokea hongo wala rushwa hivyo waliondoka eneo hilo wakimwacha mama Baraka akipambana na mumewe huku binti akiachiwa aende zake.
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: AIBU ILIYOJE: MKE AVAA KININJA, AMFUATILIA MUMEWE, AMFUMANIA
AIBU ILIYOJE: MKE AVAA KININJA, AMFUATILIA MUMEWE, AMFUMANIA
http://api.ning.com/files/ec4fSw8DDIwJcO5LgMiVzWbwUoSPGtXgCWMITD2yD6opP8*eMEhupCYOBHjirSQx5cZvVL8YXqyl1ZNf0fGgcnuF*A2PAUEk/IMG_2203.JPG
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/03/aibu-iliyoje-mke-avaa-kininja.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/03/aibu-iliyoje-mke-avaa-kininja.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy