Ikulu: Msinunue nyumba za umma
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
HomeHabariKitaifa

Ikulu: Msinunue nyumba za umma

st Updated on 26 January 2015 By Mwandishi Wetu Hits: 87 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Omben...

Serikali sasa yaalika wawekezaji wa Ghuba
Bei ya petroli, dizeli kushuka zaidi
Stars maboresho mapya yatajwa
st Updated on 26 January 2015 By Mwandishi Wetu Hits: 87


KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amewataka Watanzania kutoa taarifa kuhusu makusudio ya kuuza nyumba za Serikali na mashirika ya umma, kutokana na madeni mbalimbali ili ziweze kukombolewa kabla ya kuuzwa.

Akizungumza Ikulu Dar es Salaam juzi, Balozi Sefue alisema kumejitokeza mtindo wa kukamata nyumba za Serikali na mashirika ya umma na kuzipiga mnada, kutokana na madeni yanayodaiwa kwa Serikali au mashirika hayo.

“Sisi tumeona hii si sawa, unakuta nyumba ya Serikali inaweza kuwa na thamani labda ya Sh bilioni moja inauzwa kwa Sh milioni 100…mkiona nyumba ya Serikali inauzwa, toeni taarifa tuikomboe,” alisema.

Alisema baada ya kuikomboa, watendaji husika walioachia nyumba ya Serikali ikataka kupigwa mnada, watashughulikiwa kwa uzembe baada ya kukomboa nyumba husika.

Balozi Sefue pia aliwataka Watanzania kuepuka kununua nyumba za umma, kwa kuwa hata baada ya ununuzi, Serikali haitakubali, bali itatafuta namna ya kukomboa nyumba yake.

Hata hivyo, alikiri ugumu wa kukomboa nyumba kama imeshauzwa kisheria, kwamba ni pamoja na kufungua kesi ya kuomba kurejeshewa, utaratibu aliosema ni wa kisheria na mgumu. Kutokana na ugumu huo, alisema ndiyo maana wanaomba Watanzania kutoa taarifa mapema kabla hazijapigwa mnada ili Serikali izikomboe.

Akitoa mfano, alisema Serikali iko katika mkakati wa kukomboa jengo la Shirika la Ndege (ATCL) lililopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam, ambalo linatakiwa kupigwa mnada kulipa deni la shirika hilo. Katika hatua nyingine, Balozi Sefue alisisitiza Watanzania kuepuka kutumiwa na matapeli wanaotumia jina la Ikulu.

Alisema matapeli hao, ambao Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu ameshaongelea, wanapaswa kuepukwa.

Alitoa mfano wa watu ambao huletwa mpaka katika geti la Ikulu na mwenyeji kuingia ndani, kisha anazubaa kwa muda na kutoka na kutaka alipwe fedha kwa madai ameshafanya kazi aliyotumwa Ikulu, ikiwemo ya kutafutiwa kazi.
 
Chanzo Habari Leo
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Ikulu: Msinunue nyumba za umma
Ikulu: Msinunue nyumba za umma
http://www.habarileo.co.tz/images/resized/images/balozi-sefue25_300_173.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/ikulu-msinunue-nyumba-za-umma.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/ikulu-msinunue-nyumba-za-umma.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy