John Bocco Mshambuliaji wa Azam, John Bocco ‘Adebayor’ amekwenda Algeria kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza ...
Mshambuliaji wa Azam, John Bocco ‘Adebayor’ amekwenda Algeria kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa.
Bocco aliyerejea kwenye timu yake ya Azam hivi karibuni baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu alikuwa akisumbuliwa na majeraha ya goti na alifanya vizuri na timu hiyo kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi yaliyomalizika mwanzoni mwa wiki na Simba kutwaa ubingwa.
Mchezaji huyo yuko Algeria katika klabu ya Chabab Riadhi Baladiyat (CRB) akifanya majaribio huku klabu hiyo ikitaka kumnunua moja kwa moja kama itaridhika naye.
Mshambuliaji huyo alikwenda katika klabu hiyo ya
Ligi Daraja la kwanza mwanzoni mwa wiki hii na inaelezwa kuwa timu hiyo
inataka kumnunua moja kwa moja mchezaji huyo mwenye umbo kubwa na
anayejua kufunga mabao ya vichwa.
Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba aliliambia gazeti hili kuwa wanasubiri majibu ya klabu hiyo kuhusu mchezaji huyo na waliwapa muda hadi leo jioni kabla ya kuamua vinginevyo.
“Ni kweli Bocco yuko Algeria, kuna timu imetaka kumnunua, lakini walisema wanataka kumwona kwanza na bado tunasubiri majibu yao na tunawapa hadi kesho(leo) jioni wawe wameshatuambia nini kinaendelea,” alisema Kawemba.
Bocco aliwahi kufanya majiribio kwenye klabu ya
Supersport ya Afrika Kusini na kufuzu, lakini hata hivyo Azam iligoma
kumuuza kutokana na madai kuwa walipewa fedha kidogo.
COMMENTS