Wananchi wa familia saba za kijiji cha Sakila kilichopo kata ya kikatiti wilayani Arumeru mkoani Arusha wanal...
Wananchi
wa familia saba za kijiji cha Sakila kilichopo kata ya kikatiti
wilayani Arumeru mkoani Arusha wanalala nje na watoto wao huku
wakikabiliwa na njaa kali baada ya watu wanaodai kutumwa na serikali ya
kijiji kuvunja nyumba zao na kufyeka migomba yao.
Wakizungumza
na ITV wananchi hao wanaodai kuwa wameishi maeneo hayo kwa zaidi ya
miaka 30 wamesema wanashangazwa na viongozi wa kijiji hicho kutoa baraka
za kuvunja kwa nyumba zao kwa kisingizio kwamba wao ni wavamizi.
Mwenyekiti
wa kijiji hicho Bw Richard Mbise amesema hatua hiyo imekuja baada ya
mahakama kuthibitisha kuwa wananchi hao walivamia eneo hilo na walikiuka
taratibu.
Hata
hivyo baadhi ya viongozi wastaafu wa vijiji vya kata hiyo pamoja na
kukiri kuwepo kwa mgogoro huo wamesema hatua ya zinazochukuliwa kuutatua
zikiwemo za kuvuja nyumba na kukata migomba sio sahihi.
Tatizo
la migogoro ya ardhi katika wilaya ya Arumeru ambalo kwa sasa
linaelekea kuwa sugu limeendelea kuwaathiri wananchi wa huku baadhi ya
viongozi wakiwemo wa kisiasa wakilitumia kama ajenda za kutafuta
maslahi yao jambo ambalo lisipodhibitiwa linaweza kuleta maafa makubwa.
COMMENTS