Wasiolipa Kodi na kuendeleza maeneo waanza kubanwa
HomeHabariTop Stories

Wasiolipa Kodi na kuendeleza maeneo waanza kubanwa

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza kuwabana wamiliki wote wa ardhi wasiolipa kodi ya pango la ardhi sambamba na kutoendel...

Habari kubwa Magazetini Kenya leo July 29, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo July 28, 2024
Warembo wanaounda kundi la Tango Supreme kutumbuiza Dar usiku wa leo

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza kuwabana wamiliki wote wa ardhi wasiolipa kodi ya pango la ardhi sambamba na kutoendeleza maeneo wanayomiliki.

Wakiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa sharti la kulipa kodi na kuendeleza kwa wamiliki wa ardhi Mkoa wa Pwani tarehe 13 februari 2025, timu maalum ya ukaguzi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Mandeleo ya Makazi imesema hatua hiyo ni juhudi za wizara kukusanya kodi pamoja na kuhakikisha maeneo yanayomilikiwa na wananchi yanaendelezwa.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mapato na Uwekezaji Wizara ya Ardhi Bw. Leonard Msafiri amesema, kwa mujibu wa sheria wamiliki wa ardhi wanatakiwa kulipa kodi ya pango la ardhi na wasipofanya hivyo wanapaswa kupewa notisi ya kulipa ndani ya siku kumi na nne.

‘’Ulipaji wa kodi ya ardhi ni wajibu wa kisheria kwa mmiliki chini ya fungu 33 la sheria ya ardhi sura 113’’. Amesema


Akiwa katika shamba namba 57, 58, 59 na 60 lilipo Miswe Kibaha Mkoani Pwani, Kamishna wa Ardhi Msaidiźi Mapato na Uwekezaji Wizara ya Ardhi amemweleza mmiliki wa mashamba hayo kuwa ana nafasi ndani ya siku kumi na nne kulipa kodi ya ardhi.

Aidha, Kamishna wa ardhi Msaidizi Mkoa wa Pwani Ndg. Hussein Sadiki Iddi, ameeleza kuwa ndani ya siku hizo kumi na nne mmiliki anaweza kufika Ofisi za ardhi ili kupewa ushauri na kueweka namna nzuri ya kufanya mazungumzo ya kulipa deni linalomkabili.

Timu ya ukaguzi ilitembelea pia shamba namba 2 eneo la Miswe kata Mbwawa, halmashauri ya manispaa Kibaha ambapo mmiliki wake anadaiwa kiasi cha Tsh mil 690. Katika eneo hilo Kamishna Msafiri alielekeza mmiliki wake kupatiwa barua ya onyo ikiwa ni hatua ya kwanza ya mchakato wa ufutaji ardhi kwa mujibu wa fungu la 45 ya sheria ya ardhi sura ya 113. Barua hiyo alikabidhiwa Bw. Dunia Mrisho Kinyogoli ambaye ni mwakilishi Miswe

Vile vile, timu hiyo ilitembelea kituo cha mafuta cha ATN picha ya ndege mkoani Pwani ambapo mmiliki wake amadaiwa kiasi cha Tsh 24. Mmiliki huyo alikabidhiwa barua ya onyo kupitia Meneja wa kituo Bw. Abdallah Bawazir.

Kamishna Msafiri alieleza kuwa zoezi la kufuatilia madeni ya kodi ya pango la ardhi ni endelevu na linafanyika katika mikoa yote hivyo amehimiza wadaiwa wote wa kodi ya pango la ardhi kuhakikisha wanalipa madeni yao ili kuepuka usumbufu unaoweza kuwapata wakati wa kuendesha shughuli zao.

The post Wasiolipa Kodi na kuendeleza maeneo waanza kubanwa first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/TDZStwF
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Wasiolipa Kodi na kuendeleza maeneo waanza kubanwa
Wasiolipa Kodi na kuendeleza maeneo waanza kubanwa
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2025/02/464c41de-90fb-4399-9670-5f79fe9c21e6-950x634.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/02/wasiolipa-kodi-na-kuendeleza-maeneo.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/02/wasiolipa-kodi-na-kuendeleza-maeneo.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy