Waziri Kombo aagana na Balozi wa Marekani
HomeHabariTop Stories

Waziri Kombo aagana na Balozi wa Marekani

Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano kwa Ubalozi wa Marekani nchini na kuahidi kumpatia ushirikiano wa karibu Balozi ajaye katika utekeleza...

Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano kwa Ubalozi wa Marekani nchini na kuahidi kumpatia ushirikiano wa karibu Balozi ajaye katika utekelezaji wa majukumu yake awapo Tanzania pamoja na kuangazia maeneo ya kuongeza wigo wa ushirikiano kwa manufaa ya nchi zote mbili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, akimuaga Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Michael Battle anayetarajiwa kuondoka nchini hivi karibuni.

Waziri Kombo amemshukuru Balozi Battle kwa ushirikiano mzuri kati ya wizara na ubalozi katika kipindi chote cha uongozi wake pamoja na kufanya kazi kwa karibu na sekta na wizara mbalimbali za kimaendeleo nchini.

Aidha, ametumia fursa hii kutoa salamu za pole kwa msiba wa Rais Mstaafu wa Marekani, Hayati Jimmy Carter aliyefariki Dunia Desemba 29, 2024.

Kwa upande wake, Balozi Battle amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake katika kuleta maendeleo Tanzania lakini pia kwa utayari wake katika shughuli za ushirikiano.

Ameomba pia Wizara kumpa ushirikiano wa karibu Kaimu Balozi atayekuwepo wakati Marekani ikingoja kutuma Balozi mwingine.

 

The post Waziri Kombo aagana na Balozi wa Marekani first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/ViOnyvB
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Kombo aagana na Balozi wa Marekani
Waziri Kombo aagana na Balozi wa Marekani
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2025/01/IMG-20250109-WA0017-950x633.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/waziri-kombo-aagana-na-balozi-wa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/waziri-kombo-aagana-na-balozi-wa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy