Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi kumaliza changamoto za utitiri wa Kodi kwa wafanyabiashara.
HomeHabariTop Stories

Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi kumaliza changamoto za utitiri wa Kodi kwa wafanyabiashara.

Utitiri wa Kodi kwa wafanyabiashara ni moja ya changamoto kubwa inayosababisha kukwepa ulipaji Kodi stahiki kwa kundi hilo na kwamba jambo h...

Utitiri wa Kodi kwa wafanyabiashara ni moja ya changamoto kubwa inayosababisha kukwepa ulipaji Kodi stahiki kwa kundi hilo na kwamba jambo hilo si tu linadhohofisha maendeleo ya wafanyabiashara hao kuendesha biashara zao lakini pia linaikosesha Serikali kupata kodi inayostahili.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara na Kilimo Mkoa wa Morogoro Mwadhine Mnyanza wakati wa kikao tume ya Rais ya maboresho ya Kodi kilichofanyika mjini .Morogoro ambapo amesema wafanyabiashara hukumbana na changamoto mbalimbali zikiwemo wingi wa kodi, kubwa hasa katika sekta zinazokuwa kibiashara jambo linalopelekea kufikia hatua ya kukwepa kodi.

Myanza amesema ni vizuri Serikali ikaweka chombo Kimoja cha kukusanya Kodi ambayo itakuwa rafiki Kwa wafanyabiashara ,lakini Kila taasisi kukusanya Kodi kwenye biashara Moja inadhoofisha maendeleo Yao .

Anasema kutoka ana changamoto hiyo inawalazima wengine kukwepa Kodi ,kukimbia madeni na Kufunga biashara na kusababisha kukosekana kwa mapato.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Morogoro amesema katika eneo muhimu sana katika kuboresha mazingira ya biashara hapa Nchini ni kuangalia suala la wingi wa kodi ambalo linaweza kuwavutia wawekezaji wengi, hivyo ameiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kushirikiana katika kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kulipa kodi.

Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Maboresho ya kodi Balozi Mwanaid Maajar amesema, kilio cha wengi ni utitiri wa kodi unaotokana na uchache wa walipa kodi huku Mamlaka husika zikiwa zinaelekeza nguvu zake za kudai kodi sehemu chache ili kupata kodi jambo ambalo linamrudisha nyuma mfanyabiashara kwa sababu ya kulipa kodi nyingi.

Balozi huyo amesema.lengo la Tume hiyo kuwa kupokea malalamiko, changamoto na mapendekezo ili kuboresha mazingira ya kufanyia biashara na kuangalia namna ya kurahisisha utaratibu wa wafanyabiashara kupata leseni, kulipa tozo na kulipa kodi kwa urahisi.

Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano w Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan ameanzisha tume hiyo Ili iweze kutatua changamoto hizo hivyo wafanyabiashara wakae meza Moja na mamlaka husika Ili kumaliza changamoto hizo.

 

 

The post Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi kumaliza changamoto za utitiri wa Kodi kwa wafanyabiashara. first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/wgekMA9
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi kumaliza changamoto za utitiri wa Kodi kwa wafanyabiashara.
Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi kumaliza changamoto za utitiri wa Kodi kwa wafanyabiashara.
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2025/01/IMG-20250123-WA0009.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/tume-ya-rais-ya-maboresho-ya-kodi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/tume-ya-rais-ya-maboresho-ya-kodi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy