Elimu ya usalama wa vyombo vya usafiri majini yatolewa Mara
HomeHabariTop Stories

Elimu ya usalama wa vyombo vya usafiri majini yatolewa Mara

Tanzania imekuwa mwanachama wa Shirika la Bahari Duniani (IMO) kwa takribani miaka 50 sasa na kumekuwa na juhudi za uboreshaji wa Sera ya Ta...

Tanzania imekuwa mwanachama wa Shirika la Bahari Duniani (IMO) kwa takribani miaka 50 sasa na kumekuwa na juhudi za uboreshaji wa Sera ya Taifa ya Usafiri kwa njia ya maji unaoendelea nchini na hii imekuwa  ishara tosha ya dhamira ya serikali kuboresha usalama wa usafiri kwa njia ya maji.

Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Uchukuzi Bi. Stella Katondo  katika maadhimisho ya siku ya usafiri kwa njia ya maji na miaka 50 ya IMO kwa siku ya pili amesema katika kuona hilo elimu zaidi inapaswa kutolewa kuhusu usalama na kuwa na vifaa okozi wakiwa safarini alipotembelea wavuvi wa mwalo wa Makoko mkoani manispaa ya musoma mkoani Mara.

‘ vyombo vya usafiri majini vinatakiwa kukaguliwa kabla ya kuanza safari iwe ya Uvuvi au kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine hiyo ndio sababu wao kutoa elimu kwa wavuvi  katika mwalo huu ndio maana tumewafuata kuwapa elimu kwanini ni muhimu kuwa na vifaa vya kuokoa ”

‘Usafiri wote wa majini  katika kuwa salama wanatakiwa kuwa na vifaa kinga pale panapo tokea janga lolote kuweza kusaidia kujiokoa katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama wanavyotumia vyombo vya usafiri majini’.

Bw. Augustino Magele Kaimu kamanda zimamoto mkoani amesema kuwa ni muhimu katika  wavuvi, manahodha wa vyombo, wamiliki wa vyombo, wafanyabiashara na watumiaji wa vyombo vidogo vya usafiri majini kuipata  elimu ya jinsi ya kutumia vifaa vya uokoaji pindi inapotokea dharura au ajali majini;  utumiaji vifaa vya uokoaji pamoja  umuhimu wa kuwa na vifaa vya uokozi  kwenye vyombo vya maji.

‘kuwa vifaa vya uokozi katika safari za majini ya uvuvi na safari za kawaida huvaliwa kabla ya safari kuanza kutokana na vifaa hivyo kuendelea kuwepo bila kuvaliwa wakati janga linapotokea hakuna hata mmoja anaweza kukumbuka uwepo wa vifaa hivyo na kusababisha madhara makubwa ikiwemo na vifo lakini mnaweza kupiga mamba za dharura endapo shida ikitokea’.

Bw Mauna Shabani moja ya wavuvi waliohudhuria kupata elimu hii amepongeza na kushukuru juhudi za utoaji elimu na kuomba Shirika kuendelea kufanya hivyo mara kwa mara ili kuongeza uelewa mpana kwa wananchi juu ya sekta ya usafiri majini.

Kilele kikitarajiwa kuwa tarehe 26 Septemba 2024.

Kauli mbiu ya maadhimisho haya ni “Navigating the future:safety first”

 

 

 

The post Elimu ya usalama wa vyombo vya usafiri majini yatolewa Mara first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/Zh2l7p0
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Elimu ya usalama wa vyombo vya usafiri majini yatolewa Mara
Elimu ya usalama wa vyombo vya usafiri majini yatolewa Mara
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/09/IMG-20240925-WA0011-950x760.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/09/elimu-ya-usalama-wa-vyombo-vya-usafiri.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/09/elimu-ya-usalama-wa-vyombo-vya-usafiri.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy