Miradi 77 inaendelea kutekelezwa na Tanroads nchini
HomeHabariTop Stories

Miradi 77 inaendelea kutekelezwa na Tanroads nchini

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na utekelezaji wa mir...

Marufuku kupiga picha za viumbe hai Taliban
Habari kubwa Magazetini Kenya leo October 15, 2024
Huduma ya madaktari bingwa wa mama Samia sio sasa :RC Malima

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na utekelezaji wa miradi 77 ya ujenzi wa barabara na madaraja kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) yenye thamani ya Shilingi Trilioni 4.6.

Aidha, Serikali kupitia TANROADS tayari imekamilisha kwa asilimia 100 miradi 25 ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 1,198 iliyogharimu Shilingi Trilioni 1.68 katika kipindi cha utawala wa Rais Dkt. Samia.

Haya yamebainishwa Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Eng. Mohamed Besta wakati wa akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Dodoma (Dodoma Outer Ring Road) kwa kiwango cha lami sehemu ya pili inayoanzia Ihumwa Dry Port – Matumbulu – Nala (km 60).

Eng. Besta ameeleza tangu Rais Samia aingie madarakani ameweka kipaumbele katika ujenzi wa barabara na madaraja ili kurahisisha usafiri na usafirshaji na kwa sasa Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi 77 ya ujenzi wa barabara na madaraja yenye thamani ya takribani Triloni 4.6.

“Kazi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja inaendelea kwa kasi maeneo mbalimbali nchini na hakuna mradi uliokwama kwasababu Serikali ya Rais Samia imekuwa ikilipa wakandarasi kulingana na mikataba”, amesema Besta.

Besta ameongeza kuwa hadi sasa Shilingi Bilioni 101.1 zimelipwa kwa Makandarasi katika miradi 24 ya barabara inayoendelea kutekelezwa pamoja na miradi ya minne (4) ya ujenzi wa viwanja vya ndege nchini.

Kadhalika, Besta ameeleza kuwa ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigogo Busisi) ambalo linagharimu Shilingi Bilioni 717 limefikia zaidi ya asilimia 94.

Amefafanua kuwa kutokana na mafanikio ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja nchini imeifanya Tanzania kuwa nafasi ya 6 kati ya nchi 54 za Afrika kuwa na mtandao bora wa barabara ikipanda kutoka nafasi ya 16 iliyokuwapo katika mwaka 2022 kulingana na Takwimu za Statista.com.

The post Miradi 77 inaendelea kutekelezwa na Tanroads nchini first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/ARswmt4
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Miradi 77 inaendelea kutekelezwa na Tanroads nchini
Miradi 77 inaendelea kutekelezwa na Tanroads nchini
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/10/9d9d96e1-98b2-4282-b24f-8daded2e66a2-950x713.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/10/miradi-77-inaendelea-kutekelezwa-na.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/10/miradi-77-inaendelea-kutekelezwa-na.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy