Maendeleo ni makubwa nchini, Watanzania tumuunge mkono Rais Samia-Mathias Canal
HomeHabariTop Stories

Maendeleo ni makubwa nchini, Watanzania tumuunge mkono Rais Samia-Mathias Canal

Rasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan anapaswa kutiwa moyo na kuungwa mkono kwa maendeleo makubwa anayoyafanya...

Rasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan anapaswa kutiwa moyo na kuungwa mkono kwa maendeleo makubwa anayoyafanya kwa ajili ya watanzania sio kubezwa au kumkejeli.

Wakati Tansania inapata uhuru mwaka 1961 Tanzania ilikuwa na Chuo Kikuu kimoja ila kwa sasa ameimatisha sekta ya elimu na kuwa na vyuo vikuu 30 na vyuo vishiriki 12 mpaka sasa.

Kwenye Wilaya ya Iramba kulikuwa na shule 4 za msingi na sasa zipo za msingi 111 ambapo za serikali ni 108 na shule binafsi ni 3, kwa upande wa shule ya sekondari Wilaya ya Iramba likuwa na shule 1 na sasa zipo 29 ambapo za serikali ni 26 na za binafsi zipo 3.

 

Hayo yamebainishwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa WazoHuru Media Group Ltd Ndg Mathias Canal, tarehe 19 Septemba 2024 na Mgeni rasmi katika mahafali ya 61 ya Shule ya Msingi Kiomboi-Bomani iliyopo Wilayani Iramba katika Mkoa wa Singida na kuongeza kuwa Rais Samia ni mwanasiasa mstahimilivu na mwenye utulivu wa hali ya juu katika uongozi wake.

Mathias ameeleza kuwa mwaka 2022 serikali ilifanya mapitio na Mabadiliko ya mitaala na Sera ya elimu ya mwaka 2014 hatimaye kuwa na toleo jipya la sera ya elimu ya mwaka 2023.

Amesema kwa ujumla katika sera hiyo ya elimu kutakuwa na mambo muhimu ikiwemo Kutoa elimu ujuzi badala ya taaluma pekee, na Elimu ya lazima itakuwa miaka 10 badala ya 7.

Mathias Canal amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda kwa kuja na wazo la ujenzi wa vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) ambapo Wilaya ya Iramba imepokea Bilioni 1.4 na ujenzi wa VETA unaendelea katika Kijiji cha Salala kata ya Old Kiomboi.

Hali kadhalika amempongeza Mbunge wa Jimbo la Iramba ambaye ni Waziri wa Fedha Mhe Dkt Mwigulu Mchemba kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali nchini ikiwemo katika jimbo lake ambapo katika kipindi cha miaka minne 2020-2024 Wilaya ya Iramba imepokea Bilioni 6.682 kwa ajili ya sekta ya elimu.

Katika mahafali hayo Ndg Mathias Canal amechangia kiasi cha Shilingi 400,000 kwa ajili ya motisha kwa walimu, Mipira 6 na jezi jozi mbili. Mipira mitatu na jezi jozi moja kwa ajili ya mchezo wa mpira wa miguu (Football) na mipira mitatu na jezi jozi moja kwa ajili ya mchezo wa mpira wa pete (Netball).

 

The post Maendeleo ni makubwa nchini, Watanzania tumuunge mkono Rais Samia-Mathias Canal first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/N081rPg
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Maendeleo ni makubwa nchini, Watanzania tumuunge mkono Rais Samia-Mathias Canal
Maendeleo ni makubwa nchini, Watanzania tumuunge mkono Rais Samia-Mathias Canal
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/09/907d7bb5-749a-4b62-80d8-d10980dda6ef-950x910.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/09/maendeleo-ni-makubwa-nchini-watanzania.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/09/maendeleo-ni-makubwa-nchini-watanzania.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy