Mwenyekiti UWT akemea vikali  vitendo vya ulawiti na ubakaji kwa watoto
HomeHabariTop Stories

Mwenyekiti UWT akemea vikali vitendo vya ulawiti na ubakaji kwa watoto

Mwenyekiti wa Jumuiya Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Taifa Mary Chatanda, ameendelea kukemea vikali vitendo vya ulawiti na ubakaji kwa watot...

Habari kubwa Magazetini Kenya leo November 28, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo November 28, 2024
Wadau wapongeza BOT kwa kudhibiti wanaokiuka taratibu za kifedha

Mwenyekiti wa Jumuiya Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Taifa Mary Chatanda, ameendelea kukemea vikali vitendo vya ulawiti na ubakaji kwa watoto, huku akisisitiza mapambano dhidi ya kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia nchini.

Akiwa Jijini Mwanza Mwenyekiti huyo wa (UWT) Taifa, katika uzinduzi wa Kamati inayolenga Mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia (UWT), mkoa wa Mwanza ameeleza kuwa kwa sasa hali ni mbaya kutokana na vitendo vya ulawiti na ubakaji kushamiri kwa baadhi ya maeneo nchini, sambamba na kuwataka wazazi kutofumbia macho vitendo hivyo pale inapobainika ndugu wa karibu kuhusika.

Mwenyekiti huyo amekwenda mbali zaidi na kuwataka wanafamilia kuwa makini inapotokea wametembelewa na wageni majumbani wasiruhusu kulala nyumbani na badala yake, wawapeleke nyumba za kulala wageni, huku akisema atawashawishi Wabunge wanawake kupitisha sheria ya wanaume kuhasiwa pale inapobainika kutenda vitendo hivyo.

Halima Nassor ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mapambano dhidi ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia (UWT) mkoa wa Mwanza, anaweka bayana dhamira yao ya kutaka kuzifikia wilaya zote za Mwanza, huku akibainisha takwimu za ukatili wa kijinsia mkoa wa Mwanza.

Uzinduzi wa Kamati ya Mapambano dhidi ya kupinga Ukatili umefanyika Jijini Mwanza, ikiwa na kauli mbiu isemayo ‘Vunja minyororo ya Ukatili wa Kijinsia, Mwanza salama’.

The post Mwenyekiti UWT akemea vikali vitendo vya ulawiti na ubakaji kwa watoto first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/LJCzId0
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mwenyekiti UWT akemea vikali vitendo vya ulawiti na ubakaji kwa watoto
Mwenyekiti UWT akemea vikali vitendo vya ulawiti na ubakaji kwa watoto
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/08/ab030ebe-f9ca-413b-985e-74821052193f-950x534.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/08/mwenyekiti-uwt-akemea-vikali-vitendo.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/08/mwenyekiti-uwt-akemea-vikali-vitendo.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy