TIC YAKUTANA NA WAWEKEZAJI WA NDANI YA NCHI
HomeHabariTop Stories

TIC YAKUTANA NA WAWEKEZAJI WA NDANI YA NCHI

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Gilead Teri amesema kuwa kuboreshwa kwa sheria mpya ya uwekezaji imeibua faida mba...

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo February 3, 2025
Lugha 15 za kigeni kutoka mwanza kuwapa watanzania faida kimataifa
Habari kubwa Magazetini Kenya leo February 2, 2025

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Gilead Teri amesema kuwa kuboreshwa kwa sheria mpya ya uwekezaji imeibua faida mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupunguza kiwango cha mtaji kutoka Dola za Marekani 100.000 mpaka 50.000 kwa Watanzania ili kuwawezesha kuwekeza kwa urahisi zaidi.

Teri ameyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa wawekezaji Wazawa waliosajili miradi yao Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), uliofanyika leo Julai 25,2025 Jijini Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa mkutano huko umelenga kujadili maboresho ya  sheria ya Uwekezaji namba 10 ya mwaka 2022, sura namba 38 ambayo imeikasimisha TIC jukumu la kuratibu, kuhimiza, kuhamasisha, na kuwezesha uwekezaji Tanzania, sambamba na kuishauri Serikali kuhusu sera ya uwekezaji na mambo mbalimbali yanayohusu uwekezaji nchini.

“kuna vivutio vipya ambavyo vimewekwa kwa Watanzania ambao tayari wameshawekeza lakini wanataka kukuza uwekezaji wao, na kuboresha wawekezaji wapya.

“Tunaweza kukupatia vivutio vya uwekezaji sio tu pale unapoanza bali pia pale ambapo unaendeleza na kukuza uwekezaji wako” ameeleza.

Ameongeza kuwa mkutano huo ni fursa kwa wawekezaji hao kupata majibu kutoka kwa Taasisi zilizopo kwenye kituo cha pamoja (one stop center), ambazo ni pamoja na BRELA, NEMC, TRA, Uhamiaji, Idara ya Kazi, NIDA ambapo zitahusika katika mchakato wa uwekezaji.

Amekisisitiza umuhimu wa uwekezaji wa ndani ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa nakubainisha kuwa TIC imejipanga kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wa ndani na kuwahakikisha huduma bora zinazohitajika ili kuendesha miradi yao kwa ufanisi.

The post TIC YAKUTANA NA WAWEKEZAJI WA NDANI YA NCHI first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/mdnzTws
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: TIC YAKUTANA NA WAWEKEZAJI WA NDANI YA NCHI
TIC YAKUTANA NA WAWEKEZAJI WA NDANI YA NCHI
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/07/WhatsApp-Image-2024-07-26-at-10.33.38-5-1024x682.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/07/tic-yakutana-na-wawekezaji-wa-ndani-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/07/tic-yakutana-na-wawekezaji-wa-ndani-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy