Tanzania, Ubelgiji Zakubaliana Kuanza Mashauriano Ya Kuanzisha Ushirikiano Uboreshaji Wa Huduma Za Bandari
HomeHabari

Tanzania, Ubelgiji Zakubaliana Kuanza Mashauriano Ya Kuanzisha Ushirikiano Uboreshaji Wa Huduma Za Bandari

 Tanzania na Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji zimekubaliana kuanza mashauriano ya kuanzisha  ushirikiano katika uboreshaji wa huduma za ban...

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aongoza swala ya Eid al-Fitr kitaifa
Makamu Wa Rais Dkt. Mpango Azuru Kaburi La Hayati Dkt.magufuli Chato
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo May 14


 Tanzania na Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji zimekubaliana kuanza mashauriano ya kuanzisha  ushirikiano katika uboreshaji wa huduma za bandari nchini. Makubaliano haya yamefikiwa  wakati wa mazungumzo yaliyofanyika hivi karibuni kati ya Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji,  Mhe. Jestas Abuok Nyamanga, na Mkurugenzi Mtendaji wa Bandari ya Antwerp, Bw. Kristof  Waterschoot.  

Hatua hiyo, ni utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Mheshimiwa Alexander de Croo, wakati wa ziara aliyoifanya Rais Samia nchini Ubelgiji Februari 2022.  

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao walikubaliana juu ya umuhimu wa kuimarisha  ushirikiano zaidi katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kijamii na kiuchumi, ikiwa ni pamoja na  ushirikiano kati ya Mamlaka za Usimamizi wa Bandari Tanzania na Bandari ya Antwerp.  Bandari ya Antwerp inashika nafasi ya pili kwa ukubwa Barani Ulaya na ni miongoni mwa  bandari kubwa zaidi duniani.

Katika mazungumzo baina ya Balozi Nyamanga na Mkurugenzi Mtendaji wa Bandari ya  Antwerp, bandari hiyo imeonesha utayari wa kuanza mashauriano na Mamlaka za Usimamizi  wa Bandari Tanzania katika kuangalia maeneo ya ushirikiano yatakayolenga kuimarisha na  kuongeza ufanisi wa bandari kwenye utoaji wa huduma zake kwa kuanzia na Bandari za Dar es  Salaam na Zanzibar.  

Katika kutekeleza azma hiyo, Ujumbe wa Bandari ya Antwerp unatarajiwa kuja Tanzania kati  ya Septemba na Oktoba 2022, kwa lengo la kujionea hali halisi ya maeneo yanayohitaji  ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili ili kuleta ufanisi zaidi.  

Moja ya maeneo yanayotarajiwa kujadiliwa wakati wa ziara hiyo ni pamoja na namna ya  kuboresha usimamizi na muundo wenye tija kwa watoa huduma mbalimbali wa bandari;  uboreshaji wa miundombinu ya bandari na maeneo mengine yanayohusika na usafirishaji wa  mizigo; kuongeza uhimilivu na ushindani wa kibiashara na kujengea uwezo watumishi wa  Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari na Taasisi nyingine zinazohusika moja kwa moja katika  utoaji wa huduma za bandari nchini.

Katika eneo la mafunzo, tayari Bandari ya Antwerp imeanza kutoa mafunzo kwa watumishi wa  Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania. Kwa sasa, watumishi wanne (4) wa Mamlaka  hiyo wanaendelea na mafunzo ya muda mfupi katika Chuo cha Bandari ya Antwerp.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia balozi zake itaendelea  kutumia uzoefu na mafanikio ya taasisi mbalimbali kutoka nchi nyingine duniani kuboresha  utendaji na kuongeza ufanisi wa taasisi zake nchini, ikiwemo Mamlaka za Usimamizi wa  Bandari.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Tanzania, Ubelgiji Zakubaliana Kuanza Mashauriano Ya Kuanzisha Ushirikiano Uboreshaji Wa Huduma Za Bandari
Tanzania, Ubelgiji Zakubaliana Kuanza Mashauriano Ya Kuanzisha Ushirikiano Uboreshaji Wa Huduma Za Bandari
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjoGkJtpA46fu-vi3F9eWiLrslBSezJSYAVy8E3xMAOIXbhbisimB8giX11zDBaRnW27S1HwDWEHk-0RxV7K86N78tJO0t2ZsOv8JCyIM-7EChC8s4JKsGfSnaoYn7R5dzeBpp8FRHuvQAs2L0voQcuGfVJj_38ap79jg9Rfu4a4mPz_jpQn4PSigSAdg/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjoGkJtpA46fu-vi3F9eWiLrslBSezJSYAVy8E3xMAOIXbhbisimB8giX11zDBaRnW27S1HwDWEHk-0RxV7K86N78tJO0t2ZsOv8JCyIM-7EChC8s4JKsGfSnaoYn7R5dzeBpp8FRHuvQAs2L0voQcuGfVJj_38ap79jg9Rfu4a4mPz_jpQn4PSigSAdg/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/07/tanzania-ubelgiji-zakubaliana-kuanza.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/07/tanzania-ubelgiji-zakubaliana-kuanza.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy