Graphite Kuanza Kuchimbwa Ruangwa-Majaliwa
HomeHabari

Graphite Kuanza Kuchimbwa Ruangwa-Majaliwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ipo katika majadiliano na kampuni ya Uranex kwa ajili ya ujenzi wa mgodi wa madini ya bunyu ...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne February 10
Serikali yaombwa kusitisha tozo za utalii
Hotuba Ya Mapendekezo Ya Mwongozo Wa Maandalizi Ya Mpango Na Bajeti Ya Serikali Na Mpango Wa Maendeleo Wa Taifa Kwa Mwaka 2021/22


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ipo katika majadiliano na kampuni ya Uranex kwa ajili ya ujenzi wa mgodi wa madini ya bunyu (graphite) utakaoanza hivi karibuni.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa wananchi wa wilaya ya Ruangwa wajiandae kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zitokanazo na ujenzi wa mgodi wa graphite.

Ameyasema hayo  (Jumanne, Julai 5, 2022) wakati akizungumza na wananchi katika vijiji vya Namikulo, Namkatila na Matambarale katika kata ya Chunyu wilayani Ruangwa, Lindi.

“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kila kwenye rasilimali kabla ya kuanza uwekezaji lazima wahusika wajadiliane na Serikali ili kubaini namna ambavyo itanufaika.”

Waziri Mkuu amesema wakazi wa maeneo hayo watakuwa ndio wanufaika wa kwanza kutokana na shughuli mbalimbali zinakazokuwa zikiendelea kuanzia hatua ya ujenzi hadi uzalishaji.

“Kila shughuli itakayofanyika hapa ni fursa kwetu sisi wana-Namikulo na wana-Ruangwa kiujumla. Tujipange sawa sawa Serikali yenu ipo makini kuhakikisha mnanufaika na mradi huo.”

Kwa upande wake, Meneja wa Mradi wa kampuni ya Uranex, Mhandisi Isaac Mamboleo amesema kampuni yao inatarajia kuanza ujenzi wa mgodi huo katika mwaka huu wa fedha.

Amesema mradi huo ambao utahusisha vijiji saba unatarajia kugharimu shilingi bilioni 625 na utazalisha ajira 950 kati yake ajira 600 wakati wa ujenzi na ajira 350 wakati wa uzalishaji.

Mhandisi Mamboleo amesema kwa sasa wanakamilisha ujenzi wa nyumba 59 zenye gharama ya shilingi bilioni 3.6 kwa ajili ya kuwafidia baadhi ya wananchi waliopisha ujenzi wa mradi huo.

Amesema baada ya kukamilisha ulipaji fedha kama fidia ya ardhi na mazao, pia wanajenga nyumba zenye ubora kwa ajili ya kuwafidia wananchi 59 waliokuwa na nyumba katika eneo la mradi. “Nyumba hizo tunajenga nje ya eneo la mradi na kila mtu anajengewa nyumba kulingana na ukubwa wa nyumba yake ya awali.”

Nao, baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo wameziomba kampuni za uwekezaji zitoe kipaumbele kwa wananchi wanaoishi karibu maeneo ya mradi na kwamba wamejipanga na wako tayari kwa kazi



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Graphite Kuanza Kuchimbwa Ruangwa-Majaliwa
Graphite Kuanza Kuchimbwa Ruangwa-Majaliwa
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgT6QsitwjXotdJY9TqiNl0I7iWPXJn40PxfF1h0WTixeZL7Qa9t_cgrFLKDVuqA_B0BeMnnQv72aAyFkWdW_WkeHlKmbE4Tib3wTUb-qceR2I3iKlZ5z9BKJpo1OcAr6CnJVy5TJhcvz842QQERlwavz5se0_TAg9_egEwDW7IFwA85iADanhN0_IlzA/s16000/DSC_0973-1024x631.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgT6QsitwjXotdJY9TqiNl0I7iWPXJn40PxfF1h0WTixeZL7Qa9t_cgrFLKDVuqA_B0BeMnnQv72aAyFkWdW_WkeHlKmbE4Tib3wTUb-qceR2I3iKlZ5z9BKJpo1OcAr6CnJVy5TJhcvz842QQERlwavz5se0_TAg9_egEwDW7IFwA85iADanhN0_IlzA/s72-c/DSC_0973-1024x631.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/07/graphite-kuanza-kuchimbwa-ruangwa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/07/graphite-kuanza-kuchimbwa-ruangwa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy