Waziri Mkuu Aitaka Tamisemi Isimamie Ukusanyaji Mapato
HomeHabari

Waziri Mkuu Aitaka Tamisemi Isimamie Ukusanyaji Mapato

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Nchi (OR-TAMISEMI), Innocent Bashungwa na viongozi wengine wa wizara hiyo wahakikishe ku...

Nafasi Mpya za Kazi Serikalini,NGOs na Makampuni Binafsi
Naibu Waziri Mabula Ahimiza Uwajibikaji Sekta Ya Ardhi
Taarifa kwa Umma kuhusu maendeleo ya Chanjo ya Corona nchini.


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Nchi (OR-TAMISEMI), Innocent Bashungwa na viongozi wengine wa wizara hiyo wahakikishe kuwa suala la ukusanyaji mapato kwenye Mikoa, Halmashauri na Mamlaka za Serikali za Mitaa linapewa kipaumbele ili kuongeza mapato ya Serikali..

“Ajenda ya ukusanyaji mapato iwe ya kudumu ili yaongezeke hadi kufikia shilingi trilioni 2 kutoka makadirio ya sasa mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo Halmashauri zimekadiria kukusanya mapato ya ndani ya shilingi trilioni 1.01 ikilinganishwa na shilingi bilioni 863.85 zilizoidhinishwa kwa mwaka 2021/2022,” amesema.

Ametoa wito huo  Mei 31, 2022 alipokutana na Waziri wa TAMISEMI, Naibu Mawaziri, Katibu Mkuu, Naibu Makatibu Wakuu pamoja na Wakurugenzi na Wakuu wa taasisi za wizara hiyo kwenye kikao alichokiitisha jijini Dodoma ili kuwakumbusha wajibu wao.

“Nimekuja kwenye ziara ya kawaida ya kiutendaji ili kuzungumza na viongozi wakuu wa wizara na wakuu wa idara. Ni lazima ujitambue wewe ni nani hapa kwenye wizara, unatakiwa kufanya nini, mpango kazi wako ukoje na je ni wako peke yako ama unahitaji watu wengine ili uweze kuutekeleza,” amesema.

“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anataka kuona Watanzania wanafikiwa na huduma. Ni lazima tujiulize, je huduma hizo zinafika kwa wananchi kwa wakati. Watanzania wanaitegemea TAMISEMI kuanzia ngazi ya mkoa, wilaya, halmashauri, kata vijiji hadi vitongoji. Kwa hiyo, tunapaswa kuhakikisha hiyo chain inafanya kazi,” amesema.

Amesema watumishi hao wanapaswa kutambua kwamba bila uaminifu, uadilifu na uwajibikaji hawawezi kufanikiwa lakini pia wanapaswa kusimamia mambo hayo matatu hadi ngazi za chini

Amewapongeza viongozi na Watendaji wa wizara kwa kufanikiwa kuongeza hati safi kwenye taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) katika kipindi cha mwaka 2019/2020 na 2020/2021.

“Taarifa ya CAG kuhusu Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2020/2021 imebainisha Halmashauri 178 sawa na asilimia 96 zimepata hati safi, Halmashauri sita sawa na asilimia tatu zimepata hati zenye shaka na Halmashauri moja sawa na asilimia moja imepata hati mbaya”.

Waziri Mkuu amesema matokeo ya ukaguzi wa hesabu za mwaka wa fedha 2020/2021 yanaonesha mwenendo mzuri wa aina ya hati za ukaguzi zilizotolewa ikilinganishwa na ukaguzi wa hesabu za mwaka wa fedha wa 2019/2020 ambapo Halmashauri zilizopata hati safi zilikuwa 124 sawa na asilimia 67, Halmashauri zilizopata hati zenye shaka zilikuwa 52 sawa na asilimia 29 na Halmashauri zilizopata hati mbaya zilikuwa nane sawa na asilimia nne.

“Mwaka huu hati mbaya zimepungua kutoka nane hadi moja, kwa hiyo kama leo tumefikia asimilia 96 tuna uwezo wa kufikia asilimia 100, kutafuta ile mbaya na zenye mashaka sita zikaondoka.”

Ameitaka menejimenti ya wizara hiyo iwe na ubunifu, iongeze matumizi ya TEHAMA ili kuongeza mapato ya Serikali, Wakuu wa Idara wagawe majukumu kwa wasadizi wao na wakurugenzi wawe na vikao vya mara kwa mara na wasaidizi wao.




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Mkuu Aitaka Tamisemi Isimamie Ukusanyaji Mapato
Waziri Mkuu Aitaka Tamisemi Isimamie Ukusanyaji Mapato
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgjHLgPT36CUSXaeXiDyhage_GbQlH7KN-IOXPHfI_TUwj2I4hzSqxzFMRTHJXSb7vfp0eonaGFqjHekGVnGlrB4O4x8W_SMiU_KnF2Usn4zStvfpl8_LTKcW64uWU-wJJAF0gwtnpEv6JPjyGdhbfCuKcyXFD5sFs6NtODmLGIbZgnbvNjijVEq4HNOg/s16000/1.jpeg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgjHLgPT36CUSXaeXiDyhage_GbQlH7KN-IOXPHfI_TUwj2I4hzSqxzFMRTHJXSb7vfp0eonaGFqjHekGVnGlrB4O4x8W_SMiU_KnF2Usn4zStvfpl8_LTKcW64uWU-wJJAF0gwtnpEv6JPjyGdhbfCuKcyXFD5sFs6NtODmLGIbZgnbvNjijVEq4HNOg/s72-c/1.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/06/waziri-mkuu-aitaka-tamisemi-isimamie.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/06/waziri-mkuu-aitaka-tamisemi-isimamie.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy