Serikali Inaifanyiakazi Changamoto Ya Msongamano Wa Magari Mpaka Wa Tunduma
HomeHabari

Serikali Inaifanyiakazi Changamoto Ya Msongamano Wa Magari Mpaka Wa Tunduma

Farida Ramadhani, WFM, Dodoma Serikali imeahidi kuendelea kutatua changamoto ya msongamano wa magari katika Kituo cha Forodha Tundum...

Waziri Bashungwa: Wakandarasi Wazembe Kutopatiwa Kazi Za Tarura
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo January 23
Balozi Mulamula Afanya Mkutano Kwa Njia Ya Simu Na Waziri Wa Mambo Ya Nje Wa Sweden


Farida Ramadhani, WFM, Dodoma

Serikali imeahidi kuendelea kutatua changamoto ya msongamano wa magari katika Kituo cha Forodha Tunduma ikiwemo kuangalia uwezekeno wa kuongeza kituo kingine.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande alipojibu swali la Mbunge wa Momba, Mhe. Condester Michael Sichwale aliyetakakujua wakati ambao Serikali itaongeza geti jingine ndani ya Jimbo la Momba kutokana na geti la Tunduma kuzidiwa katika kutoa huduma.

Mhe. Chande alisema katika kurahisisha biashara kati ya Tanzania na Zambia na kuondoa changamoto ya msongamano wa magari katika Kituo hicho cha Tunduma, Serikali inaendelea kuchambua na kutathmini taratibu zilizopo ili kuona kama kuna uwezekano wa kuongeza Kituo cha Forodha.

“Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuondokana na changamoto ya msongamano wa magari ambapo Januari 2021, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliingia makubaliano na Mamlaka ya Mapato Zambia yanayoelekeza hatua mbalimbali za kuchukua kwa kila nchi”, alisema.

Alizitaja hatua hizo kuwa ni kuunganisha mfumo wa TANCIS wa TRA na mfumo wa ASCUDA World wa Zambia ili kuiwezesha Idara ya Forodha Zambia kupata taarifa za shehena ya mzigo husika kabla ya kuwasili mpakani, na Serikali ya Zambia kufanya maboresho ya miundombinu ya barabara na eneo la kuegesha magari kupitia ufadhili wa TMEA (Trademark East Africa).

Mhe. Chande alisema pamoja na makubaliano hayo, Serikali kwa upande wa Tanzania ilianzisha Kituo cha Pamoja cha Forodha (One Stop Border Post, OSBP) ambacho kimesaidia taasisi zote za Serikali kuwa sehemu moja na kuwasiliana kwa haraka.

Alisema pia kuwa Serikali kupitia ufadhili wa TMEA imenunua scannerstatu (3) ambazo ni baggage scanner, body scanner na cargo scanner. Aidha, baggage scanner na body scanner zinafanya kazi na cargo scanner inatarajiwa kuanza kufanya kazi mwezi Julai 2022.

 

Mwisho.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Serikali Inaifanyiakazi Changamoto Ya Msongamano Wa Magari Mpaka Wa Tunduma
Serikali Inaifanyiakazi Changamoto Ya Msongamano Wa Magari Mpaka Wa Tunduma
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgwiXqsArAlZ4gsTpeBu3mHaSWilT9BbItdDgyDeT82WB6v7uQgzaHvKyupx6bAicuLbmP1kbRBUlKLQiTsTkmX2kUiPZdukRo-RctRRSRj2KxqaG7GiFw1ZT3hrfETerFG99neuEB1SlGHkXOams5jhCOdxekI2-3V884gPD1GHW3ZI4s9wKzfIwTvqQ/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgwiXqsArAlZ4gsTpeBu3mHaSWilT9BbItdDgyDeT82WB6v7uQgzaHvKyupx6bAicuLbmP1kbRBUlKLQiTsTkmX2kUiPZdukRo-RctRRSRj2KxqaG7GiFw1ZT3hrfETerFG99neuEB1SlGHkXOams5jhCOdxekI2-3V884gPD1GHW3ZI4s9wKzfIwTvqQ/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/06/serikali-inaifanyiakazi-changamoto-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/06/serikali-inaifanyiakazi-changamoto-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy