Putin: Tumezuia Nchi za Magharibi kuivamia Urusi kwa kuanzisha oparesheni ya kijeshi Ukraine
HomeHabari

Putin: Tumezuia Nchi za Magharibi kuivamia Urusi kwa kuanzisha oparesheni ya kijeshi Ukraine

Rais Vladimir Putin wa Russia ametetea oparesheni za kijeshi ambazo nchi yake ilianzisha dhidi ya Ukraine na kusema ilibidi afanye hivyo ...

Picha:Rais Samia akizindua ndege za mafunzo ya awali ya marubani na mabasi kwa JWTZ
Kwa uwekezaji huu bandari ya Dar es Salaam itakuwa yamfano wa kuigwa -CPA Chalamila
Habari kubwa Magazetini Kenya leo August 29, 2024


Rais Vladimir Putin wa Russia ametetea oparesheni za kijeshi ambazo nchi yake ilianzisha dhidi ya Ukraine na kusema ilibidi afanye hivyo kwani nchi za Ulaya zilikuwa zinapanga kuishambulia Russia kijeshi.

Putin ameyasema hayo katika hotuba wakati wa gwaride la kila mwaka la Siku ya Ushindi katika Medani Nyekundu mjini Moscow leo Jumatatu kwa munasaba wa kukumbuka ushindi wa Shirikisho la Sovieti dhidi ya Ujerumani ya Kinazi katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Akifafanua zaidi, Rais Putin amesema: "Nchi za Magharibi zilikuwa zinajitayarisha kuvamia ardhi yetu, likiwemo eneo la Crimea, na hivyo oparesheni ya kijeshi (nchini Ukraine) ilikuwa hatua ya kuzuia uvamizi."

Putin amesema nchi za muungano wa kijeshi wa NATO zilikataa kusikiliza ilichokuwa ikikisema Russia jambo lililoashiria zilikuwa zinapanga njama na kwa msingi huo Russia ilichukua uamuzi wa kuzuia hujuma dhidi yake huku akisema uamuzi wake wa oparesheni za kijeshi nchini Ukraine ulikuwa wa nguvu na kwa wakati muafaka.

Aidha amesema uamuzi huo wa oparesheni za kijeshi dhidi ya Ukraine ulikuwa sahihi kwani nchi hiyo ilikuwa inapokea silaha za kisasa kabisa kutoka muungano wa kijeshi wa NATO.

Rais wa Russia amefichua kuwa Ukraine ilikuwa inapanga kujizatiti kwa silaha za nyuklia na hivyo nchi yake haikuwa na budi ila kuanzisha oparesheni za kijeshi dhidi ya Kiev ili kusambaratisha njama hizo.

Russia ilianzisha oparesheni za kijeshi dhidi ya Ukraine mwezi Februari baada ya nchi hiyo kukataa kutekeleza mapatano ya Minsk na pia baada ya maeneo ya Donetsk na Luhansk kujitangazia uhuru ambao ulitambuliwa rasmi na Moscow.




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Putin: Tumezuia Nchi za Magharibi kuivamia Urusi kwa kuanzisha oparesheni ya kijeshi Ukraine
Putin: Tumezuia Nchi za Magharibi kuivamia Urusi kwa kuanzisha oparesheni ya kijeshi Ukraine
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiw2shzdletfHuh0VQhFbB6LJroEaPsNSDlH9z34Afxt7w0jF7ehjBnGUY-UZtGiXf1kxd0zERY-nH7ZRNzthFsaqJ_lk0-pjR2NS76i1lHmRXAZfSsVENnDsa8PilwWzoR00J4BupNg57pNqZo2mUSiW53p1jgV5TV7imqFpBl6DTwmVGIE3bmy0kSCw/s16000/2.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiw2shzdletfHuh0VQhFbB6LJroEaPsNSDlH9z34Afxt7w0jF7ehjBnGUY-UZtGiXf1kxd0zERY-nH7ZRNzthFsaqJ_lk0-pjR2NS76i1lHmRXAZfSsVENnDsa8PilwWzoR00J4BupNg57pNqZo2mUSiW53p1jgV5TV7imqFpBl6DTwmVGIE3bmy0kSCw/s72-c/2.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/05/putin-tumezuia-nchi-za-magharibi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/05/putin-tumezuia-nchi-za-magharibi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy