Serikali Yatoa Fursa Kwa Wanafunzi Kubadili Combination
HomeHabari

Serikali Yatoa Fursa Kwa Wanafunzi Kubadili Combination

  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amesema wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne ...

TIC YAKUTANA NA WAWEKEZAJI WA NDANI YA NCHI
Habari kubwa Magazetini Kenya leo July 26, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo July 26, 2024

 


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amesema wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2021 wanayo nafasi ya kubadili machaguo ya tahasusi (Combination) na kozi mbalimbali wanazohitaji kusoma kulingana na ufaulu wao.

Kauli hiyo ameitoa  Machi  29,2022 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari Waziri Bashungwa amesema, hatua hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi waliohitimu Kidato cha Nne kutokujaza fomu (Selfom) kwa uhakika wakati wanachagua combination zau kozi zao kutokana na kutokuwa na uhakika wa ufaulu katika masomo yao.

“Ofisi ya Rais -TAMISEMI imekamilisha zoezi la awali la kuingiza kwenye kanzi data taarifa zilizo kwenye fomu za mwanafunzi kama zilivyojazwa na wanafunzi wakiwa shuleni, hii inazoa nafasi kwa wanafunzi kuweza kufanya mabadiliko ya machaguo yao” amesema Bashungwa

Aidha amesema kuwa Serikali imetoa fursa kwa wahitimu wa Kidato cha Nne kubadili machaguo yao ili kutoa nafasi zaidi kwa mwanafunzi kusoma tahasusi au kozi itakayomwandaa kuwa na utaalam ambao unaendana na machaguo yake hapo baadae.

“Amewataka wazazi kushiriki kikamilifu na kukubaliana na mwanafunzi katika zoezi hili ili pasiwepo na malalamaiko yoyote ya mwanafunzi kuwa amepangiwa machaguo ambayo hakuyachagua hapo baadae” amesema Waziri Bashungwa

Hata hivyo amefafanua kuwa zoezi la kubadilisha tahasusi kwa mwanafunzi linafanyika kwa utaratibu wa kuingia kwenye mfumo wa uchaguzi wa wanafunzi (student Selection MIS) kupitia kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz kwa kutumia namba ya mtihani.

Waziri Bashungwa ametoa ushauri kwa wazazi,walezi na wanfunzi kuendelea kutumia dawati la huduma kwa wateja kupitia barua pepe helpdesk@tamisemi.go.tz au na kituo cha huduma kwa wateja kwa simu namba +255 262 160 20 na +255 735 260 210 au fika katika ofisi za Mamlaka za Serikali za Mitaa.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Serikali Yatoa Fursa Kwa Wanafunzi Kubadili Combination
Serikali Yatoa Fursa Kwa Wanafunzi Kubadili Combination
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgYc0TP_U-1kHx6Iscv2FMh8jUWVoL0ZE6xzoHQwoZHxVtzbSrhfrjWGKthR9I2m1yDYRs98QakOU1cj8JxnU5p4hGnuS4tlcKQXhHJ2Zc7Dpp5DdRwN9V7eYiRUPfbc-dvzV6Io54-jYAisWBmETSQxGRucMujBOeogiHcG3sajY2hMQ8mlXwiZSlV9Q/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgYc0TP_U-1kHx6Iscv2FMh8jUWVoL0ZE6xzoHQwoZHxVtzbSrhfrjWGKthR9I2m1yDYRs98QakOU1cj8JxnU5p4hGnuS4tlcKQXhHJ2Zc7Dpp5DdRwN9V7eYiRUPfbc-dvzV6Io54-jYAisWBmETSQxGRucMujBOeogiHcG3sajY2hMQ8mlXwiZSlV9Q/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/03/serikali-yatoa-fursa-kwa-wanafunzi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/03/serikali-yatoa-fursa-kwa-wanafunzi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy