Tanzania Kuwavutia Wawekezaji Kwenye Siku Ya Tanzania Maonesho Ya Expo 2020 Dubai
HomeHabari

Tanzania Kuwavutia Wawekezaji Kwenye Siku Ya Tanzania Maonesho Ya Expo 2020 Dubai

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kuendelea kuwavutia Wawekezaji kwenye Siku maalum ya Tanzania kwenye Maonesho ya E...

Serikali Yatoa Tsh bilioni 100 Kupunguza Bei ya Mafuta
Rais Samia kufanya ziara ya siku mbili Uganda
Rais Samia Suluhu Akutana Na Kuzungumza Na Mwenyekiti Wa Chadema Freeman Mbowe Ikulu Jijini Dar Es Salaam


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kuendelea kuwavutia Wawekezaji kwenye Siku maalum ya Tanzania kwenye Maonesho ya Expo 2020 Dubai ambapo lengo la siku hiyo ni kuitangaza nchi ya Tanzania kwenye Maonesho hayo makubwa Duniani yanayoshirikisha nchi 192.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara tarehe 01 Februari , 2022 Jijini Dar es Salaam wakati akiongoza kikoa cha Maandalizi ya Siku ya Tanzania kwenye Maonesho ya Expo 2020 Dubai kilichoshirikisha viongozi wa Taasisi za Serikali na Sekta Bianfsi.

Prof. Godius Kahyarara amesema kuwa Siku ya hiyo inalenga kutangaza miradi mikubwa ya uwekezaji hivyo amezitaka Taasisi zinazoshiriki kwenye Siku hiyo kuhakikisha zinakuwa na taarifa kutosha za miradi ili kuwashawishi wakezaji kuwekeza nchini.

Prof. Kahyarara ameongeza kuwa sisi kama waandaaji tunapaswa kuwa na taarifa za kutosha na za kina za fursa za uwekezaji zilizopo nchini ili kupata wawekezaji kuja kuwekeza nchini Tanzania na sio kutoa taarifa ambayo haijitoshelezi.

“ Taasisi zote zifanye maandalizi mazuri ya kutangaza fursa katika miradi mbalimbali ili ilete manufaa makubwa kwa nchi yetu kupitia Siku hiyo na Kongamano la Biashara ambalo litawakutanisha wawekezaji na wafanyabiashara ” alisema Prof. Godius Kahyarara

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Latifa Khamis ambao ndio waratibu wa ushiriki wa Tanzania kwenye Maonesho hayo alieleza kuwa kwenye Maonesho ya EXPO 2020 Dubai kila Nchi inapewa fursa ya kuandaa Siku ya Kitaifa kwenye Maonesho hayo ili kujitangaza ambapo siku maalum ya Tanzania itakuwa tarehe 26 Februari, 2022 na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Bi. Latifa ameongeza kuwa kwenye siku hiyo mgeni Rasmi anatarajiwa kutembelea Banda la Tanzania, Banda la Wanawake (Women Pavilion) pamoja na banda la “ Nature Pavilion “ na siku hiyo itapambwa na burudani kutoka kwa wasanii wa Tanzania na anatarajiwa kuhudhuria kwenye Kongamano la Biashara na Uwekezaji linalotarajiwa kufanyika siku ya Tarehe 27 Februari, 2022 ambapo, atahutubia na kushuhudia utiaji wa saini wa mikataba ya Biashara na Uwekezaji kwenye Kongamano hilo.

Aidha Bi. Latifah amesema Kongamano hilo litatoa tathmini ya tulichofanikiwa katika Maonesho hayo ya Expo 2020 Dubai toka yalipoanza tarehe 01 Oktoba, 2021 na litatoa fursa kwa Wafanyabiashara wa Tanzania kukutana na Wafanyabiashara kutoka Nchi mbalimbali sambamba na kuendelea kutangaza fursa za uwekezaji zinazopatikana Nchini Tanzania.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bi. Angelina Ngalula amesema Siku hiyo sio ya Serikali peke yake ni shughuli ya Kitaifa ambayo Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi zinapaswa kushirikiana katika kupanga ajenda zitakazotoa nafasi kwa Sekta Binafsi kuunganishwa na fursa za Biashara na Uwekezaji.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Tanzania Kuwavutia Wawekezaji Kwenye Siku Ya Tanzania Maonesho Ya Expo 2020 Dubai
Tanzania Kuwavutia Wawekezaji Kwenye Siku Ya Tanzania Maonesho Ya Expo 2020 Dubai
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgzm58OsGdYIwfkhmStoAHic7wTdZRhFKEnKZq8m5xTHRN-P16fRlrVBJMwtRw1N03DJj3mgVEx8K-bTxQG8V4Xl9RjgJskmhZ_DcwutyDhkYrBysylEJReMkaNWKUh9QzBkCg32MxvFNcqdgmasj2BsxVDzAqO-JqOINWIKpGd1BU6jkZqEeDKwHwCvQ=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgzm58OsGdYIwfkhmStoAHic7wTdZRhFKEnKZq8m5xTHRN-P16fRlrVBJMwtRw1N03DJj3mgVEx8K-bTxQG8V4Xl9RjgJskmhZ_DcwutyDhkYrBysylEJReMkaNWKUh9QzBkCg32MxvFNcqdgmasj2BsxVDzAqO-JqOINWIKpGd1BU6jkZqEeDKwHwCvQ=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/02/tanzania-kuwavutia-wawekezaji-kwenye.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/02/tanzania-kuwavutia-wawekezaji-kwenye.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy