Waziri Wa Fedha Mwigulu Nchemba Ateta Na Mkurugenzi Wa Benki Ya Kiarabu (Badea)
HomeHabari

Waziri Wa Fedha Mwigulu Nchemba Ateta Na Mkurugenzi Wa Benki Ya Kiarabu (Badea)

Na Benny Mwaipaja, Dodoma WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amefanya mazungunzo kwa njia ya mtandao na ...

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo September 27, 2024
Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa taasisi zinazosimamia maswala ya usafiri majini
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo September 26, 2024


Na Benny Mwaipaja, Dodoma
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amefanya mazungunzo kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA) Dr. Sidi Ould Tah, kujadili namna ya kuharakisha upatikanaji wa fedha za mkopo nafuu na msaada unaokadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 3 sawa na takriban shilingi za Tanzania trilioni 7 zitakazotolewa na Benki hiyo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Akizungumza katika mkutano huo uliowashirikisha pia Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Dkt. Nchemba alisema kuwa Serikali imeazimia kuuelekeza mkopo huo kwenye miradi 32 iliyoko Bara na Visiwani katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo cha umwagiliaji, maendeleo ya mifugo, upanuzi wa miundombinu ya Chuo Kikuu-Zanzibar (SUZA) na uwezeshaji wa Serikali za Mitaa.

Aidha, Dkt. Nchemba alibainisha kuwa pamoja na uwekezaji wa fedha hizo katika miradi ya kimkakati itakayosaidia kukuza ajira na kuharakisha ukuaji wa uchumi wa nchi, mkopo na misaada hiyo itasaidia kuendeleza sekta binafsi kwa njia ya ukuzaji biashara ya uagizaji kwa sekta binafsi na usafirishaji wa bidhaa kwa taasisi za kifedha nchini.

Aliwaagiza wataalam mbalimbali Serikali ikiwemo Wizara ya Kilimo kuainisha sehemu ya eneo la Hekta milioni 29 linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji kwa kuwa na maandiko ya kitaalam yanayohusu maeneo hayo ili yaweze kupatiwa fedha.

Naye Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe alisema kuwa fedha kutoka BADEA zitasaidia kuendeleza miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji kwenye miradi 19 ili kuongeza tija katika eneo la umwagiliaji linalokadiriwa kufikia hekta milioni 1.2 kati ya Hekta milioni 29 zilizopo hivi sasa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA) Dr. Sidi Ould Tah, alisema Benki yake imejipanga kutoa kiasi hicho cha fedha cha dola za Marekani bilioni 3 na kwamba atatuma timu ya wataalam kutoka Benki hiyo kuja nchini itakayoungana na timu ya  wataalam wa ndani ili kujadili kwa kina zaidi  namna ya kutekeleza mpango huo.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Wa Fedha Mwigulu Nchemba Ateta Na Mkurugenzi Wa Benki Ya Kiarabu (Badea)
Waziri Wa Fedha Mwigulu Nchemba Ateta Na Mkurugenzi Wa Benki Ya Kiarabu (Badea)
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEh6b-ZTT3WJcppMY8ENaHqmY__K2Fq8DCxTkEngdicv2SvZ-N01CriSbJnVVFXgWN5Gtsjgryd0Y6Si56m4TfWLWpyRx_vkYGq-n2OiJgJa2qziQe6KlVauej7x9iQm0YzTIZO8AaUOVTWxmMLWPakByObFhIW7zzo-yezRmSuiDRHR8tF61ETPkP21OQ=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEh6b-ZTT3WJcppMY8ENaHqmY__K2Fq8DCxTkEngdicv2SvZ-N01CriSbJnVVFXgWN5Gtsjgryd0Y6Si56m4TfWLWpyRx_vkYGq-n2OiJgJa2qziQe6KlVauej7x9iQm0YzTIZO8AaUOVTWxmMLWPakByObFhIW7zzo-yezRmSuiDRHR8tF61ETPkP21OQ=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/waziri-wa-fedha-mwigulu-nchemba-ateta.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/waziri-wa-fedha-mwigulu-nchemba-ateta.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy