Waziri Mkenda Avitaka Vyuo Vya Ufundi Kuwa Na Mitalaa Ya Kuzalisha Wanafunzi Watakaoweza Kujiajiri Ama Kuajiriwa
HomeHabari

Waziri Mkenda Avitaka Vyuo Vya Ufundi Kuwa Na Mitalaa Ya Kuzalisha Wanafunzi Watakaoweza Kujiajiri Ama Kuajiriwa

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amevitaka Vyuo vya  Ufundi kuhakikisha vinakuwa na mitalaa itakayowezesha  kuza...

Ajali mbaya yatokea Geita usiku wa kuamkia leo
Habari kubwa Magazetini Kenya leo November 17, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo November 17, 2024


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amevitaka Vyuo vya  Ufundi kuhakikisha vinakuwa na mitalaa itakayowezesha  kuzalisha wanafunzi watakaoweza kujiajiri ama kuajiriwa katika soko la ndani na nje ya nchi.

Prof. Mkenda amesema hayo Januari 26, 2022 Jijini Arusha alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) ambapo amesema ili kuwawezesha wanafunzi wanaomaliza katika Vyuo hivyo  ni lazima mitaala ikidhi vigezo vya elimu ya ufundi vya kimataifa.

Waziri huyo amesema Mitaala ya Vyuo vya Ufundi lazima iwawezeshe wanafunzi kujiamini katika  kujiajiri ama kufanya kazi nje ya mipaka ya nchi na itoe wanafunzi wenye uwezo wa kutumia vifaa na mitambo ya kisasa kwa kuwa Sayansi na Teknolojia duniani inakua kwa haraka sana.

“Uhuishaji wa mitaala ya Vyuo vya Ufundi nchini ni lazima uangalie mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi pamoja na kuhakikisha vinafikia viwango vya kimataifa  ili kuwezesha vijana wanaopata mafunzo kuwa na maarifa, stadi na ujuzi unaokubalika kimataifa,” amesisitiza Prof. Mkenda.

Aidha, Prof. Mkenda ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa miradi mbalimbali Chuoni hapo ikiwemo ujenzi wa bweni la wasichana litakalohudumia wanafunzi 600, ujenzi wa kituo cha afya na umaliziaji wa jengo la Ufundi Tower ambalo ujenzi wake ulisimama kwa muda mrefu.

Akielezea maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ufundi Tower linalojengwa kwa fedha za UVIKO 19, Msimamizi wa mradi wa ujenzi huo Mhandisi Faraji Magania amesema kwamba chuo kimetengewa Shilingi bilioni 2.25 ili kukamilisha ujenzi huo.

“Katika gawio ambalo tumelipata la Shilingi bilioni 1.75 zitatumika kumalizia shughuli za ujenzi na katika hiyo Shilingi milioni 500 zitanunua samani ambazo itajumuisha na vifaa vya kufundishia. Jengo hili baada ya kukamilika litakuwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi 1,100 kwa wakati mmoja,” amefafanua Mhandisi Magania.

Katika hatua nyingine Prof. Mkenda amevitaka Vyuo vya Ufundi kuendelea kuboresha mafunzo ya sayansi na teknolojia kwa kupeleka Wakufunzi kusoma nje ya nchi kwenye vyuo vikubwa ili waweze kujifunza zaidi jinsi nchi hizo zilivyofanikiwa katika kutoa mafunzo hayo na wao waweze kuboresha mbinu za kutoa mafunzo.

“Nchi zote ambazo zimeendelea, zimefanikiwa kwa kupeleka watu wao kwenda kujifunza nje hasa katika maeneo ya sayansi, teknolojia na tiba, tungependa kuona chuo hiki walimu na wakufunzi wake wanakwenda kuona kinachoendelea na kujifunza kwenye vyuo vikubwa nje ya nchi,” alisema Prof. Mkenda.

Waziri huyo amesisitiza kuwa Wizara na Serikali kwa ujumla itatenga fedha kwa ajili ya kupeleka Wakufunzi nje ya nchi ili wapate mafunzo ambayo yatawezesha kutoa elimu ya kisasa na yenye kujenga ujuzi kwa vijana wa Kitanzania.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Mkenda Avitaka Vyuo Vya Ufundi Kuwa Na Mitalaa Ya Kuzalisha Wanafunzi Watakaoweza Kujiajiri Ama Kuajiriwa
Waziri Mkenda Avitaka Vyuo Vya Ufundi Kuwa Na Mitalaa Ya Kuzalisha Wanafunzi Watakaoweza Kujiajiri Ama Kuajiriwa
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEhVW-7bpEiOhZwpyC0TeMu1Hkvs_5uTpGI7WRxzlvC1Sv1AkJ5LoFLBny0Wm5ViGqfdmhRbmNXLTNWcN1F4MAgSIJm13YQmvv4OQR2EjqU6T2rmrtEHdWHIu3qaV5T8diTNl75NmEGwM05I5zkCTkEyTLQ_bO9WBXOr0Lh7whceEm2yjPVSjteaXnJMkA=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEhVW-7bpEiOhZwpyC0TeMu1Hkvs_5uTpGI7WRxzlvC1Sv1AkJ5LoFLBny0Wm5ViGqfdmhRbmNXLTNWcN1F4MAgSIJm13YQmvv4OQR2EjqU6T2rmrtEHdWHIu3qaV5T8diTNl75NmEGwM05I5zkCTkEyTLQ_bO9WBXOr0Lh7whceEm2yjPVSjteaXnJMkA=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/waziri-mkenda-avitaka-vyuo-vya-ufundi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/waziri-mkenda-avitaka-vyuo-vya-ufundi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy