Prof. Mbarawa Awataka Bandari Kujipanga Ubora Wa Miundombinu
HomeHabari

Prof. Mbarawa Awataka Bandari Kujipanga Ubora Wa Miundombinu

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kusimamia miradi ya miundombin...

Nafasi 15 za Kazi Management and Development for Health (MDH) ......Mwisho wa Kutuma Maombi ni 19th October 2021.
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo October 11
Kijana Auawa na Baba Yake Mzazi Baada Ya Kutorosha Binti kwa Mila za Kisukuma za "Chagulaga" Na Kumtambulisha Kama Mke


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kusimamia miradi ya miundombinu kikamilifu kwa kwa kuweka mikakati maalum ya kuitembelea na kufanya vikao vya mara kwa mara ili kuwezesha miradi hiyo kukamilika kwa wakati na viwango.

Akizungumza Mkoani Kigoma  baada ya kukagua mradi wa upanuzi wa bandari za Kibirizi na Ujiji Prof. Mbarawa ametoa rai kwa TPA kupitia upya miradi ya wanayotekeleza nchini kote na kwa kuchukua hatua stahiki ikiwemo kuongeza idadi ya wahandisi kweye miradi hiyo.

“Mamlaka ina miradi nchi nzima lakini miradi niliyotembelea leo ya bandari za ziwa Tanganyika imekuwa ikisuasua sana, mhandisi mshauri anaandika barua ya vikao TPA hamuonekani, kwa namna hii hatutafika na sio sawa’ Amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amebainisha kuwa kukamilisha kwa miradi hiyo kutarahisisha shughuli za usafirishaji baina ya Kigoma na nchi Jirani zinazozunguka Mkoa huo ikiwemo Jamhuri ya Kidekrasia ya Kongo (DRC) na Burundi kwani kupitia bandari hizi usafirishaji utarahisishwa.

Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua maendeleo ya ukarabati ya Meli ya MT Sangara na kuitaka Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kusimamia mradi huo kwa kukagua kila hatua ya ukarabati huo ili kupata thamani ya fedha na kuepuka kufungiwa vipuri visivyokidhi vigezo kulingana na mkataba.

Naye Meneja wa Bandari ya Kigoma, Manga Gasaya amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa ndani ya wiki mbili kuanzia sasa tathmini itafanyika na Mamlaka itatoa taarifa ya mikakati iliyojiwekea kukamilisha miradi hiyo ikiwemo ratiba za ukaguzi.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Allen Butembelo amesema ukarabati wa meli ya MT. Sangara umefikia asilimia 40 na kuahidi kuendelea kuusimamia ili ukamliike kwa wakati.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa yuko Mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo pamoja na mambo mengine atashiriki kikao kitakachowakutanisha Mawaziri wa Ujenzi na Uchukuzi na Fedha wa Tanzania na Burundi kujadili miradi ya maendeleo hususani Reli ya Uvinza-Musongati-Gitega.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Prof. Mbarawa Awataka Bandari Kujipanga Ubora Wa Miundombinu
Prof. Mbarawa Awataka Bandari Kujipanga Ubora Wa Miundombinu
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEhW6hbyNJ89RPRtNOQvK94iQlQ4E3Wy_Eavw_znL9N7cZeY4c4tUcgEP83ZYvFSoz0-da_30_hgAygvhMPBY2Bd-pNggVTCWijFKtfp0LyEJF5wlUZt_cA4dw-WYfsudnEYYlP7aRQUILKAsTEM7RsdjOl2bKE4KBVUVHfu-8FV6rkVaeu0rd0lOBo5Hw=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEhW6hbyNJ89RPRtNOQvK94iQlQ4E3Wy_Eavw_znL9N7cZeY4c4tUcgEP83ZYvFSoz0-da_30_hgAygvhMPBY2Bd-pNggVTCWijFKtfp0LyEJF5wlUZt_cA4dw-WYfsudnEYYlP7aRQUILKAsTEM7RsdjOl2bKE4KBVUVHfu-8FV6rkVaeu0rd0lOBo5Hw=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/prof-mbarawa-awataka-bandari-kujipanga.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/prof-mbarawa-awataka-bandari-kujipanga.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy