Korea Kaskazini imesema kwamba imefanikiwa kufyatua kombora liendalo kasi zaidi katika juhudi zake za kuimarisha mifumo yake ya kimkakat...
Korea Kaskazini imesema kwamba imefanikiwa kufyatua kombora liendalo kasi zaidi katika juhudi zake za kuimarisha mifumo yake ya kimkakati ya silaha siku chache baada ya kiongozi wake Kim Jong Un kuapa kuimarisha majeshi yake licha ya changamoto zilizosababishwa na janga la corona.
Shirika kuu la habari la Korea Kaskazini limesema kamati kuu ya chama tawala imesema imeridhishwa sana na matokeo ya jaribio hilo la jana lililofuatiliwa kwa karibu na maafisa wandamizi ya masuala ya silaha.
Jaribio hilo linaashiria kwamba taifa hilo litaendeleza mipango yake ya kuunda kombora la kisasa zaidi na wala halifikirii kurejea kwenye mazungumzo ya kuachana na mipango hiyo hivi karibuni.
Hili ni jaribio la pili kwa taifa hilo kujaribu kombora linalokwenda kasi zaidi tangu jaribio la kwanza la Septemba mwaka jana.
Credit: MPEKUZI
Thanks for your time please share with your friends
COMMENTS