Bashungwa:”Mikakati Ya Serikali Ni Kuisaidia Tanzanite Kuiondosha Ethiopia”
HomeHabari

Bashungwa:”Mikakati Ya Serikali Ni Kuisaidia Tanzanite Kuiondosha Ethiopia”

 Na. Projestus Binamungu ,WUSM Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ameliagiza Shirikisho la Mpira wa Miguu nch...

Taasisi Za Umma Zaagizwa Kutumia Mfumo Wa TANePS
Tangazo la nafasi za kazi za Makarani na Wasimamizi wa Sensa 2022
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo May 06


 Na. Projestus Binamungu ,WUSM
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ameliagiza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuhakikisha wanaiwekea mazingira wezeshi timu ya Taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 Tanzanite  yatakayowajenga kimwili na kisaikolojia wachezaji hao katika kuikabili timu ya taifa ya Ethiopia January 2022.

Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo Desemba 21, 2021 alipokutana nao na kufanya mazungumzo na wachezaji pamoja na kamati ya ufundi ya timu hiyo kujadili na kufanya tathimini ya changamoto mbalimbali za kimichezo zilizojitokeza wakiwa nchini Burundi wakati wa mchezo baina ya Tanzanite na wenzao wa timu ya wanawake ya Burundi ya chini ya umri wa miaka 20.

Waziri Bashungwa amesema kazi ya Serikali katika sekta ya michezo ni kuweka mazingira wezeshi kwa wanamichezo na timu zote zinazoipeperusha bendera ya taifa, na ndoto ya Serikali ni kuwaona wachezaji na timu zao wakiibuka washindi katika michezo yote.

Pamoja na kuelezea matamanio hayo ya Serikali, Waziri Bashungwa ameipongeza timu ya Tanzanite katika mchezo wao dhidi ya Burundi uliochezwa Desemba 18, 2021 na kuibuka na sare ya bao moja licha ya kucheza wakiwa pungufu.

“Kwa kweli mliishangaza Afrika na dunia huko Burundi, yaani mnacheza pungufu lakini bado tukapata ushindi wa heshima, kwa kweli tunawapongeza sana vijana wetu” amesema Waziri Bashungwa.

Awali akielezea baadhi ya changamoto walizokabiliana nazo huko Burundi, Mkuu wa msafara wa timu ya Tanzanite Bukuku Mrisho amesema, licha ya sheria za mpira kutaka majibu ya vipimo vya magonjwa mbalimbali kuwasilishwa masaa mawili kabla ya mchezo lakini wao waliletewa majibu ya vipimo vya Uviko 19 wakiwa uwanjani tayari na hata wakati mchezo ukiendelea wataalamu waliendelea kuleta majibu ya vipimo kwa viongozi mbalimbali wa timu.

“Yaani wakati mchezo unaendelea waliendelea kutuletea makaratasi waliyo ya kuandikwa kwa mkono kwamba fulani majibu yanaonesha ana Uviko 19, sisi tunaamini nia yao ilikuwa ni kututoa mchezoni lakini tulipambana na upungufu wetu huo huo mpaka mwisho wa mchezo tukaibuka na sare ya goli moja” amesema Mrisho.

Tanzinite inashiriki michezo hiyo ya awali kupata tiketi ya kufuzu kushiriki mashindano ya kombe la dunia yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2022 nchini Costa Rica .


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Bashungwa:”Mikakati Ya Serikali Ni Kuisaidia Tanzanite Kuiondosha Ethiopia”
Bashungwa:”Mikakati Ya Serikali Ni Kuisaidia Tanzanite Kuiondosha Ethiopia”
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjHiJWlTdJEhEiSLiU6Dd8mHhr41uKKBTYr0BKbq1vuAoY2y2dJOCzue2wepwXkYesySHfYt2Nzq9DmOlyU6o3EszpeCVtzYn0BSf1FKWtZ-jjNgi_auivPAHjK_g5zIXKAM-f_djhYFIn8jxGCw6CCICULCn3dpZjpogEFbdxMOc125gVBso6nCGegSg=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjHiJWlTdJEhEiSLiU6Dd8mHhr41uKKBTYr0BKbq1vuAoY2y2dJOCzue2wepwXkYesySHfYt2Nzq9DmOlyU6o3EszpeCVtzYn0BSf1FKWtZ-jjNgi_auivPAHjK_g5zIXKAM-f_djhYFIn8jxGCw6CCICULCn3dpZjpogEFbdxMOc125gVBso6nCGegSg=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/bashungwamikakati-ya-serikali-ni.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/bashungwamikakati-ya-serikali-ni.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy