Waziri Silaa azindua kampeni ya SITAPELIKI,itapambana na utapeli
HomeHabariTop Stories

Waziri Silaa azindua kampeni ya SITAPELIKI,itapambana na utapeli

Waziri wa mawasiliano na Teknolojia ya Habari ameongoza kikao kazi cha pili serikalini na wadau wa sekta ya mawasiliano na teknolojia ya hab...

Rais Samia na Dr. Leakey kutunukiwa Tuzo Arusha
Gavu ataka kasi zaidi kuongeza wanachama jumuiya za chama
Habari kubwa Magazetini Kenya leo December 17, 2024

Waziri wa mawasiliano na Teknolojia ya Habari ameongoza kikao kazi cha pili serikalini na wadau wa sekta ya mawasiliano na teknolojia ya habari kuhusu utekelezaji wa mkakati wa taifa wa uchumi wa kidigitali 2024/2034 kilicho fanyika hii leo jijini Arusha.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Silaa ameeleza Mafanikio ambayo kama wizara wamefikia ikiwemo ufikishwaji wa mkongo wa mawasiliano ya taifa, kukua kwa huduma za simu kiganjani , kupungua kwa garama za kupiga simu na kuwezesha huduma za kidigitali kuwafikia wafanyabiashara wengi.

Aidha katika kikao hicho Waziri Silaa akafanya uzinduzi wa kampeni ya kupambana na kuzuia utapeli kwenye mtandao kampeni ijulikanayo kama SITAPELIKI. yenye lengo la kutoa elimu kwa jamiii hususani katika kushuhulikia maswala ya utapeli na ulaghai mtandaoni. huku akihimiza wananchi kuwa na amani katika kututumia mtandao

Pia amewahimiza wananchi juu ya utaratibu wa kuwasilisha malalamiko yao kwa watoa huduma kuwa ni kupitia namba 100 pekee kwa mitandao yote au kwa malalamiko mengine wafike ofisi za TCRA.na Baada ya uzinduzi akatoa rai kwa Kila mdau kutekeleza kwa wakati mpango huo mahususi kwa kuelimisha jamiii jinsi ya kujikinga na udanganyifu wa mitandaoni

Kwa upande wake Miraji Mtaturwa mwakilishi wa mwenyekiti wa kamati bunge miundominu na mawasiliano na teknolojia akashauri Kuimarisha uwezo wa data, Malipo ya kidigitali, pamoja na Garama za bando ili kutoa urahisi wa huduma na kuweza kuwafikia wananchi wote hadi wa hali za chini.

Aidha ameongeza kuwa kupitia kikao hicho wanatarajia kulenga upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kuchochea uchumi wa kidigitali kwa kuwezesha miundombinu ya kidital, Utawala na mazingira wezeshi, Uelewa wa kidigital na ujuzi,Utamaduni wa maendeleo ya teknolojia pamoja na kukuza ushirikishwaji wa huduma za kidigitali

NaeKatibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohammed Khamis Abdulla Akaeleza kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau wameweza kufanya utekelezaji wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano ambapo hadi sasa umefikia asilimia 50 huku minara 304 imeongezwa nguvu kutoka 2G kwanda 3G, 4G na 5G ambapo utekelezwaji huo umefanikiwa kufanyika kwa asilimia 100.

Aidha akieleza mafanikio mengine wameweza kupeleka WIFI katika maeneo ya umma na mashuleni nchini, na kukamilisha majadiliano kati ya serikali na watoa huduma za mawasiliano ambapo inatarajiwa umoja wa watoa huduma wa mawasiliano kukabidhi miundombunu ya mkongo wa mawasiliano wa serikali pamoja na kusaini mkataba na serikali.

Baaada ya kikao kazi hicho kutaandaliwa maazimio ya utekelezaji wa pamoja kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, na mpango wa kufanya utafiti ufuatiliaji pamoja natathimini.

 

The post Waziri Silaa azindua kampeni ya SITAPELIKI,itapambana na utapeli first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/XULcgGw
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Silaa azindua kampeni ya SITAPELIKI,itapambana na utapeli
Waziri Silaa azindua kampeni ya SITAPELIKI,itapambana na utapeli
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250221-WA0009-950x633.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/02/waziri-silaa-azindua-kampeni-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/02/waziri-silaa-azindua-kampeni-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy