Agizo La Serikali Kuhusu Matumizi Ya ‘seal’ Kwenye Chupa Latekelezwa
HomeHabari

Agizo La Serikali Kuhusu Matumizi Ya ‘seal’ Kwenye Chupa Latekelezwa

Agizo la Serikali la kusitisha utengenezaji na uwekaji wa plastiki laini (seal) kwenye mifuniko ya chupa za maji limeendelea kutekelezwa...

Makamu Wa Rais Dkt. Mpango Afanya Mazungumzo Na Dkt. Kikwete
Vijana Waanisha Changamoto Tano Wanazopitia
Waziri Wa Nishati Afanya Mazungumzo Na Totalenergies


Agizo la Serikali la kusitisha utengenezaji na uwekaji wa plastiki laini (seal) kwenye mifuniko ya chupa za maji limeendelea kutekelezwa tangu lilipotolewa Oktoba 11, 2021 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo.

Hayo yamebainika  Desemba 21, 2021 wakati wa ziara ya Waziri Jafo ya kufuatilia maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na Serikali kuhusu utunzaji wa mazingira.

Ametembelea na kukagua kiwanda cha Watercom kinachozalisha maji ya Afya na cha Tanzania Ruidar Co. Ltd kinachojihusha na urejelezaji plastiki na kuzalisha mabomba vilivyopo eneo la Kisarawe II katika Manispaa ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

Alisema Serikali ilitoa maelekezo hayo kutokana na seal hiyo haiwezi kurejelezeka na inachafua mazingira pindi inapotupwa na kuzagaa ovyo hali inayoweza kusababisha vifo vya mifugo na samaki baharini wanapomeza.

Waziri huyo alibainisha kuwa pamoja na maelekezo hayo ya Serikali bado kuna baadhi ya kampuni bado hazijatekeleza huku akisisitiza kuwa ifikapo tarehe ya mwisho ya marufuku hiyo maji yatakaendelea kuwekewa seal hiyo yatapigwa marufuku sokoni.

Aidha, aliwatoa wasiwasi wananchi wanaodhani kuwa bila matumizi ya viplastiki hivyo kuna uwezekano wa maji kuchakachuliwa akisema kuwa matumizi ya mhuri wa moto unasaidia kuondoa changamoto hiyo.

“Nimekuja hapa kwenye kiwanda hiki cha maji na nimefarijika sana kuona tayari wameshaanza kutekeleza agizo hilo hawaweki tena viplastiki vile na wanatumia mtambo maalumu wa kuweka stamp (mhuri) na huyu ametambua umuhimu wakupila kodi kwa hiyo huwezi kununua maji hayo hadi yawe na mhuri huo,” alisema.

Kwa upande wake Bw. William Mhavila kutoka kitengo cha uzalishaji cha kampuni hiyo alisema hivi sasa wanatekeleza agizo la Serikali kwa kusisitisa uzalishaji wa vifuko hivyo.

“Kama mnavyoona tumezima mtambo huu uliokuwa unazalisha zile seal za plastiki na hivyo tumeanza kutekeleza agizo la Serikali ili tuweze kutunza mazingira,” alisema Mhavila.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo alifanya ziara katika kiwanda cha Tanzania Ruidar Co. Ltd kinachojihusisha na urejeleshaji wa plastiki na kuzalisha mabomba.

Akiwa kiwandani hapo alionesha kuridhishwa na utekelezaji wa agizo lake la miezi mitatu kwa kampuni hiyo la kurekebisha mfumo wa uchujaji wa majitaka ambao ulitiririsha majitaka kwenye makazi ya watu.

Waziri Jafo alisema kuwa kiwanda hicho kimetekeleza agizo hilo kwa asilimia mia moja na kuwataka wengine waige mfano huo kwa mustakabali wa kulinda mazingira yetu.

Pia alielekeza maafisa mazingira kufuatilia viwanda mbalimbai katika eneo hilo la Kigamboni kuona namna gani wanatimiza matakwa ya kisheria katika suala zima la utunzaji wa mazingira.

Kwa upande wake Meneja wa kiwanda hicho, Bi. Zhang Ping alisema kutokana na hatua hiyo hivi sasa anarejeleza majitaka tofauti na awali alikuwa akinunua mara kwa mara hivyo kupunguza gharama.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Agizo La Serikali Kuhusu Matumizi Ya ‘seal’ Kwenye Chupa Latekelezwa
Agizo La Serikali Kuhusu Matumizi Ya ‘seal’ Kwenye Chupa Latekelezwa
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEh5ldB0QccFO3Z7fT-E-EG1nHn9axzQhbh-bMuPDVKieqmjK4nDii1TUGViSZNNF8VPnF6-jeo5XVBkGUG0RqU4zurrRMFBbiJMcPIB1KxGCl80OIRFiNXFhmlK-rwj0csQ1tVFSxMt9hT8V15Vw0bkn7Fh1hrPD0ow4F-gU96Z3GOdVbEsFfF09XlRKA=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEh5ldB0QccFO3Z7fT-E-EG1nHn9axzQhbh-bMuPDVKieqmjK4nDii1TUGViSZNNF8VPnF6-jeo5XVBkGUG0RqU4zurrRMFBbiJMcPIB1KxGCl80OIRFiNXFhmlK-rwj0csQ1tVFSxMt9hT8V15Vw0bkn7Fh1hrPD0ow4F-gU96Z3GOdVbEsFfF09XlRKA=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/agizo-la-serikali-kuhusu-matumizi-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/agizo-la-serikali-kuhusu-matumizi-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy