Uviko-19 Usitusahaulishe Tahadhari Ya Magonjwa Mengine – Dkt. Sichalwe.
HomeHabari

Uviko-19 Usitusahaulishe Tahadhari Ya Magonjwa Mengine – Dkt. Sichalwe.

Na Atley Kuni, WAMJW-MOROGORO. Mganga Mkuu wa Serikali, Dr. Wedson Sichalwe, amesema Pamoja na kuendelea na mapambano dhidi Uviko-19, Wa...

Habari kubwa Magazetini Kenya leo September 14, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo September 14, 2024
Dkt Tulia ahitimisha mkutano wa 10 wa wabunge vijana wanachama wa umoja wa mabunge duniani


Na Atley Kuni, WAMJW-MOROGORO.
Mganga Mkuu wa Serikali, Dr. Wedson Sichalwe, amesema Pamoja na kuendelea na mapambano dhidi Uviko-19, Wataalam wa Afya hawapaswi kuacha kuendelea na juhudi za kuwa na tahadhari na kufanya tafiti za magonjwa mengine ili kuweza kuwaepusha wananchi na magonjwa ya milipuko ikiwepo Mafua makali ya virusi.

Akifungua Mkutano wa mwaka wa Ufuatiliaji wa magonjwa ya mlipuko ikiwemo mafua makali na virusi vingine vinavyoathiri  mfumo wa njia ya hewa Dkt. Sichalwe, amewaambia wataalam hao wa Afya kutoka kwenye vituo 15 vya kutolea huduma kuwa, kwa sasa magonjwa ya mlipuko hayapigi hodi, hivyo kila mara lazima wataalam wawe macho kusoma na kufanya tafiti mbalimbali zitakazo saidia kuzuia kabla hayajatokea.

“Tuna kila sababu ya kuendeleza ufuatiliaji wa magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa   kwakujenga uwezo wataalam wa nchi yetu kubaini aina ya virusi vilivyopo na pia endapo kitatokea kirusi kipya, lakini ugonjwa wa UVIKO- 19 hauondoi uwezekano wa kutokea mlipuko wa mafua inayotokana na kirusi kipya, Endapo mlipuko wa UVIKO-19 utapungua au kukoma kabisa itahitajika kuendelea na ufuatiliaji wa ugonjwa huo ( Post pandemic surveillance) kwani Mafua na UVIKO-19 vina dalili zinazoshabihiana hivyo ufuatiliaji magonjwa ni muhimu” amesema Dkt. Sichalwe.

Dkt. Sichalwe, ametoa wito kwa viongozi kusimamia ufuatiliaji kwakuwa karibu ili kuweza kuikinga jamii  na majanga ya magonjwa yenye kusababisha mlipuko, huku akiwataka wataalamu waendelee kujengewa uwezo wa kufanya ufatiliaji wa magonjwa na usimamizi shirikishi ufanyike ili kujenga uwezo wa nchi yetu kubaini magonjwa ya mlipuko mapema na kudhibiti ili kupunguza madhara na vifo hapa nchini.

Awali akielezea malengo ya Mkutano huo wa siku tatu Dkt. Vida Mmbaga, alisema, utawawezesha kupata mrejesho wa vipimo na tafiti zilizofanyika kipindi cha nyuma, “kila kituo kitapata fursa yakuelezea uzoefu wake kwa kipindi cha mwaka mzima na uzoefu uliopatikana sambamba na changamoto walizokumbana nazo.

“Aidha kikao hiki kitatumia fursa hiyo kipima ubora wa takwimu zinazopatikana maabara kwa vituo vyote kumi na vitano vinavyo shiriki mkutano huo” alisema, Dkt. Vida Mmbaga

Naye Mwakilishi kutoka kituo cha Ufuatiliaji Magonjwa cha Marekani ofisi ya Tanzania, Macelina Mponera, ameishukuru Serikali, kwa kuendelea kushirikiana nao hata kufanikisha ujenzi wa maabaara ya taifa ya jamii.

Mkutano wa mwaka wa viongozi na watendaji wa ufuatiliaji wa ugonjwa wa Mafua makali ya virusi na Virusi vingine vinavyo athiri Mfumo wa hewa  unafanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 22 hadi 24 Novemba, 2021 na kuhudhuria na wataalam wa Afya kutoka Vituo 15.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Uviko-19 Usitusahaulishe Tahadhari Ya Magonjwa Mengine – Dkt. Sichalwe.
Uviko-19 Usitusahaulishe Tahadhari Ya Magonjwa Mengine – Dkt. Sichalwe.
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEhtMc9HIf5xxmnqTAPRviMxKdphCdF4CqRQMpc-YvjzVzowEKIh8hhRnH0wduF9Lbm2_eQkVHOPPKvr-eeNwj_panuzxxgBWXU5DQs-1F6TUsAE2dxLBBw1bVqr7KTJ9Tt5hdFYjt9UJM2n-rz9Lhl9AdkoTUMoWHIbhUKO9DqSJ1SPFzM4eHO4N9fhzg=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEhtMc9HIf5xxmnqTAPRviMxKdphCdF4CqRQMpc-YvjzVzowEKIh8hhRnH0wduF9Lbm2_eQkVHOPPKvr-eeNwj_panuzxxgBWXU5DQs-1F6TUsAE2dxLBBw1bVqr7KTJ9Tt5hdFYjt9UJM2n-rz9Lhl9AdkoTUMoWHIbhUKO9DqSJ1SPFzM4eHO4N9fhzg=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/11/uviko-19-usitusahaulishe-tahadhari-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/11/uviko-19-usitusahaulishe-tahadhari-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy