Prof. Mkumbo Awataka Tbs Kuweka Mpango Wa Kuwapatia Elimu Na Nembo Za Ubora Wajasiriamali Na Wafanyabishara Wadogo .
HomeHabari

Prof. Mkumbo Awataka Tbs Kuweka Mpango Wa Kuwapatia Elimu Na Nembo Za Ubora Wajasiriamali Na Wafanyabishara Wadogo .

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo amelitaka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuweka mpango maalum wa kusaidia Wajasiria...

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Kuanza Kuwafuatilia Wadaiwa Sugu
Rukwa: Waliokula Shilingi Milioni 932 za Halmashauri Kufikishwa Mahakamani
Rais Dk. Mwinyi Awapongeza Madaktari Bingwa Wa Upasuaji Wa Ubongo Na Mishipa Ya Fahamu


Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo amelitaka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuweka mpango maalum wa kusaidia Wajasiriamali wadogo na Wafanyabiashara ndogo na za kati (SMEs) ili kuwainua kwa kuwapatia elimu ya uzalishaji wa bidhaa bora zinazokidhi viwango na kuwapatia nembo za ubora.

Prof. Mkumbo ameyasema hayo katika hafla ya utoaji wa tuzo za ubora kwa washindi wa mwaka 2020 na ufunguzi wa mashindano ya tuzo za kitaifa za ubora kwa mwaka 2021 iliyofanyika makao makuu ya TBS , Ubungo Dar es salaam. Novemba 15, 2021

“TBS muweke na mpango maalum wa kuwafundisha, kuwaelimisha Wajasiriamali wadogo na Wafanyabiashara ndogo (SMEs) wajue namna ya kuzalisha bidhaa bora na namna ya kupata nembo ya ubora, punguzeni urasimu wa kuwatambua na kuwapa idhibati” amesema Prof. Kitila Mkumbo

Prof. Mkumbo amesema kuwa kufuatia makubaliano baina ya wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) tuzo za ubora zilianzishwa ili kutambua na kukuza sekta ya biashara kupitia ubora na bidhaa na huduma katika ukanda huu.

Amesema tuzo hizi ni sehemu ya mipango ya Serikali kuendelea kuboresha huduma na bidhaa zinazozalishwa nchini katika kuhakikisha kuwa huduma na bidhaa zinakidhi viwango vya kitaifa, kikanda na kimataifa na kuweza kuhumili soko la ushindani kidunia.

Aidha, Prof. Mkumbo amebainisha kuwa tuzo zipo katika maeneo makuu mawili ambayo ni washiriki wadogo na wa kati na washiriki wakubwa vilevile zipo katika makundi makubwa matano ambayo ni Kampuni bora ya mwaka, bidhaa bora ya mwaka, huduma bora ya mwaka, muuzaji bora wa bidhaa nje na tuzo binafsi kwa mtu aliyechangia katika kuendeleza viwango vya ubora katika SADC.

Wakati huo huo, Prof. Mkumbo ametoa tuzo kwa washindi wa mashindano ya tuzo za ubora kwa mwaka 2020 ambao ni mshindi wa Kampuni bora ya mwaka ni Geared Consulting Engineering, Mshindi wa bidhaa bora ya mwaka ni Zanzibar Milling corporation Ltd na Lilian Production Group na Mshindi binafsi aliyechangia katika kuendeleza viwango vya ubora katika SADC ni Kezia Mbwambo.

Vilevile, Prof. Mkumbo amemetoa wito kwa makampuni na wadau wote kushiriki kwenye tuzo hizo hususani wale ambao hawakuwahi kushiriki ili nchi yetu iweze kupata wawakilishi katika mashindano ya tuzo kwenye Jumuiya ya Maendeleo kwa nchi za kusini mwa Afrika (SADC).

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania, Dkt. Athuman Ngenya ameeleza kuwa malengo ya kuanzisha tuzo hizo ni pamoja na kuwatambua na kuwapongeza watu binafsi pamoja na taasisi zinazofanya vizuri kwenye masuala ya ubora wakati wa utekelezaji wa shughuli zao za uzalishaji bidhaa na utoaji huduma.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Prof. Mkumbo Awataka Tbs Kuweka Mpango Wa Kuwapatia Elimu Na Nembo Za Ubora Wajasiriamali Na Wafanyabishara Wadogo .
Prof. Mkumbo Awataka Tbs Kuweka Mpango Wa Kuwapatia Elimu Na Nembo Za Ubora Wajasiriamali Na Wafanyabishara Wadogo .
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEiUZtW83zpVtr-BYkF2dpwqqK-v_8K0qW9-UcsZ1UcBPiBE7OdjXfdV8dhnB8cQPYAbIrI2mkANTjcszTA1M5iWvPs7cgCadlpYSl1obdNGeTmTtsHLi-wjoRm4qWRTimNNDAnSgqh81DHEoMKj8uO_riNNh-vN_yMflf0VklubvOTjUa4aRzZHflvdRQ=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEiUZtW83zpVtr-BYkF2dpwqqK-v_8K0qW9-UcsZ1UcBPiBE7OdjXfdV8dhnB8cQPYAbIrI2mkANTjcszTA1M5iWvPs7cgCadlpYSl1obdNGeTmTtsHLi-wjoRm4qWRTimNNDAnSgqh81DHEoMKj8uO_riNNh-vN_yMflf0VklubvOTjUa4aRzZHflvdRQ=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/11/prof-mkumbo-awataka-tbs-kuweka-mpango.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/11/prof-mkumbo-awataka-tbs-kuweka-mpango.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy